TANGAZO


Friday, November 1, 2013

Niger kuzuia maafa Jangwani Sahara

 






Jangwa la Sahara

Waziri wa mambo ya nje wa Niger, anasema kuwa wanawake na watoto huenda wakapigwa marufuku kusafiri nje ya nchi kupitia eneo la Kaskazini mwa nchi.
"Nitapendekezea katika mkutano wetu ujao, kuwa watoto na wanawake wapigwe marufuku kuondoka nchini humo kupitia kaskazini mwa nchi,’’Bazoum Mohammed aliambia BBC.

 
Aliyasema hayo baada ya miili 92 ya wahamiaji waliofariki kutokana na kiu kupatikana katika jangwa la Sahara.
Niger iko katika mkondo ambao unatumiwa sana na wahamiaji ulio kati ya Kusini mwa jangwa la Sahara na Ulaya.

Lakini miongoni mwa wanaofanikiwa kusafiri safari hiyo ndefu huishia kuwa wafanyakazi wahamiaji katika kanda ya Afrika Kaskazini.
"Wengi wa watu hawa walitoka katika mikoa ya Niger na walikuwa wanaelekea Algeria kwenda kuomba omba katika barabara za nchi hiyo,’’ alisema waziri Mohammed.

"Wengi wanaondoka nchini humo kwa sababu ya umasikini na kuingia katika hali hii ngumu zaidi ya maisha yao ya kawaida, lakini kama tujuavyo sisi hii sio suluhu ya matatizo yao.

Waliopatikana wiki hii walikuwa wanawake na watoto wao wakienda kutafuta ajira nchini Algeria.
Bwana Mohammed alisema kuweka marufuku hiyo ndio njia ya pekee ya kusitisha mkasa kama huu kutokea tena.
Miili ya wahamiaji hao ilipatikana na waokozi baada ya gari lao kuharibikia njiani katika jangwa la Sahara.

No comments:

Post a Comment