Mamia ya waandamanaji nchini Kenya wamewasilisha kwa polisi
hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka msichana huyo wa miaka
16.
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume na kutupwa katika shimo la choo
ambapo alivunjika uti wa mgongo wake.Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.
Waandamanaji hao wameelezea kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili kumtendea haki msichana huyo.
Pia wanataka polisi waliowaadhibu washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.
Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.
Kampeini hii imekuja baada ya msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.
Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi.
No comments:
Post a Comment