Mratibu wa mbio ndefu za Uhuru Marathon, Innocent Melleck, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokua akielezea kuhusu matayarisho ya kujisajili kwa mbio hizo, unaoanza kesho katika vituo 13 jijini Dar es Salaam na kisha Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma Jumanne na Jumatano, wiki ijayo, ambapo kwa washiriki wa mbio za Kilomita 3, watalipa sh. 100,000 kwa fomu, km 5, atalipa sh. 2,000 na km 2, kulipa sh. 6,000. Kushoto ni mmoja wa wakereketwa wa mbio hizo, Mroki Mroki 'Father Kidevu'.
Mratibu wa mbio ndefu za Uhuru Marathon, Innocent Melleck, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokua akielezea kuhusu matayarisho ya kujisajili kwa mbio hizo, unaoanza kesho katika vituo 13 jijini Dar es Salaam na kisha Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma Jumanne na Jumatano, wiki ijayo.
Mratibu wa mbio ndefu za Uhuru Marathon, Innocent Melleck, akionesha moja ya fomu za kujisajili kwa ajili ya mbio hizo, unaoanza kesho katika vituo 13 jijini Dar es Salaam na kisha Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma Jumanne na Jumatano, wiki ijayo, ambapo kwa washiriki wa mbio za Kilomita 3, watalipa sh. 100,000 kwa fomu, km 5, atalipa sh. 2,000 na km 2, kulipa sh. 6,000. (Picha zote kwa hisani ya Ahamad Michuzi)
Uhuru Marathon
Mbio hizi ambazo lengo lake kubwa ni kudumisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania zina tarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam hapo Desemba 8, mwaka huu ambapo zitaanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders club.
Tuna penda kutangaza rasmi kwamba usajili kwa ajili ya mbio hizo umeanza rasmi katika Mkoa wa
Dar es Salaam, ambapo kuna vituo zaidi ya 13
vilivyofunguliwa katika maeneo mbalimbali.
Kingine mtu anayetaka kushiriki anaweza pia kujisali kwa njia ya mitandao ya kijamii kama www.uhurumarathon.com,
issamichuzi.blogspot.com, jiachie, mtaakwamtaa.blogspot.com, fazakidevu.blogspot.com, kajuna
son.blogspot.com, rweyunga.blogspot.com na nyinginenyiingi.
Aidha tunafanya utaratibu maalumu wa kuhakikisha pia yoyote anayetaka anaweza kujisaili kwanjia ya simu ya mkononi.
Katika usajili huo, fomu zitakazotolewa zitauzwa kwa bei ifuatayo; kwa mshiriki wa kilo mita 3, atalipia Sh. 100,000, yule wa kilo mita 5, Sh 2,000 na washiriki wa kilo mita 21 na 42 watalipia Sh. 6,000.
Kama ambavyo tumezungumza awali kuwa kesho zoezi hili linaanza rasmi kwa fomu kuanza kuuzwa na leo hii nawajulisha Watanzania wenzangu kuwa fomu namba moja
ya mbio za Km3 itakuwa maalumu kwa mkuu wetu wa nchi Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha watanzania kutambua kwa vitendo umuhimu wa kuenzi umoja, mshikamano na amani iliyopo pasipo kujali itakadi zozote zile,
Pia spika wabunge letu tukufu
Anna makinda yeye atachukua fomu namba mbili, fomu namba tatu itapekwa kwa Mheshimiwa
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA na mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na fomu nyingine hadi fomu namba 100
zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wetu mbalimbali wa vyama vya kisiasa,
viongozi wa dini zote na viongozi wa serikali na mashirika binasi.
Nawaomba watanzania wenzangu muwapokee vijana maalumu watakaoanza kazi ya kuuza fomu hizi katika maofisi na mashirika mbalimbali na kwa watu binafsi ili kuweza kufikia lengo kuu
la kufanya mbio zenye kutia fora na tija kwa Taifa letu.
Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo zina nia kubwa ya kutukumbusha wajibu wetu wa kutunza na kulinda amani,
umoja na mshikamano miongoni mwetu kama walivyo asisi waasisi waTaifa hili.
Kwa muda sasa tumesikia na kuona chokochoko za watu wasiolitakia mema Taifa letu kutaka kutuvuruga, sasa huu ni wakati wa kukumbushana kwamba amani iliyopo si yakuichezea wala kuifanyia majaribio inatakiwa tuipiganie kwa nguvu zote.
Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuziomba kampuni
au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo,
kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea,
hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote.
Pia tunazidi kuomba vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje
ya nchi yetu kujitokeza katika kutoa fursa kwetu kuweza kuweka matangazo ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuenzi amani iliyopo kwa vitendo pasipo kuona haya katika hili.
Tunachukua nafasi hii pia kusisitiza kuungana mkono juhudi zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika kuleta amani ndani ya Taifa hili.
Kumbuka Tanzania
ni Yetu Sote na Amani Kwanza.
Munguibariki Tanzania
Innocent Melleck.
Mratibu Uhuru marathon
No comments:
Post a Comment