TANGAZO


Friday, October 25, 2013

Serikali na Kituo cha Demokrasia wakutana kujadili Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba

Baadhi ya Wawakilishi wa Serikali wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, (kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angela Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Frederick Werema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge ), Mhe. William Lukuvi (Mb), kikao hicho kimefanyika  leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
Baadhi ya Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni  wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao hicho kimefanyika  leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Serikalini (kushoto) na Wajumbe kutoka  Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni (Kulia)  wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao hicho kimefanyika  leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Maalum.

SEREKALI imekutana  na Kituo cha Demokrasia nchini
ambacho wanachama wake ni vyama vyenye wawakilishi Bungeni  ili Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ambayo vyama hivyo viliyawasilisha Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013.

Akiongea wakati wa kikao hicho leo, Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge ), Mhe. William Lukuvi (Mb) alifafanua kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili na kuchambua Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ambayo waliombwa wayawasilishe rasmi.

“Kikao hiki  kinafanyika kufuatia kikao alichofanya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete tarehe 15 Oktoba Ikulu Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Vyama vyenye wawakilishi Bungeni na kuwaomba wawasilishe rasmi maoni yao Serikalini na sasa kamati ya kitaalam ya Serikali tumekutana nao kujadili na kuchambua Mapendekezo yao” alisema Lukuvi.

Vyama vya Siasa  vilivyo shiriki katika kikao hicho ni; CCM, CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi, UDP na TLP, kwa upande wa Serikali iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Waziri wa Sheria na Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Msaidizi wa Sheria wa Rais, Msaidizi wa Sheria wa Waziri Mkuu na Mkurugenzi wa  Idara ya Siasa na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment