TANGAZO


Friday, October 25, 2013

SUMATRA yawataka wamiliki na madereva wa Pikipiki na Bajaji kuzingatia Sheria na Kanuni za usafirishaji

Mkurugenzi Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Gilliard Ngewe akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Kanuni za Kudhibiti Usafiri wa Pikipiki na Bajaj, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Fatma Salum.
Mkurugenzi Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Gilliard Ngewe akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) mtoa huduma ya usafiri wa Pikipiki akiwa amekiuka sheria kwa kumpakia abiria pasipo kuvaa kofia ngumu (HELMENT) na kupakia abiria zaidi ya mmoja, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Maelezo, Fatma Salum.
Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akitoa wito kwa wamiliki wa Pikipiki na madereva wa usafiri huo, kushirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza Sheria na kanuni zilizowekwa na mamlaka hiyo, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)

MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imewataka wamiliki na madereva wa pikipiki na Bajaji kufuaata na kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa barabara Gilliard Ngewe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Ngewe amewataka wamiliki na waendesha vyombo hivi  kuzingatia wajibu wao  kwa kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani wa kuhakikisha wanaheshimu sheria, na kudhibiti vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria na kulinda usalama wao na abiria wao.
Aliongeza kuwa ni vyema wamiliki wakatambua masharti ya Leseni zao ambayo aliyataja kuwa ni kwanza pikipiki husika kutoa huduma katika eneo lililoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na lazima pikipiki husika zikidhi viwango vya shirika la viwango.
Alifafanua zaidi kuwa dereva wa pikipiki haruhuswii kubeba abiria zaidi ya mmoja ambapo kwa pikipiki za miguu mitatu zinatakiwa kubeba abiria kama inavyotakiwa kwa mujibu wa leseni zao zinazowapa kibali cha kubeba abiria wasiozidi watatu.
Pia Dereva wa pikipiki anatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga na kuwa na alama ya eneo analofanyia  biashara ya kubeba abiria. Ngewe alisema

Ngewe aliongeza kuwa abiria wanatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga wakati wote wanapotumia usafiri  wa huo ili kuepusha  madhara yanayoweza kuwapata mara ajali inapotokea.

Naye Meneja mawasiliano  wa Mamlaka hiyo David Mziray alisema wanashirikiana na mamlaka nyingine  kama  halmashauri za miji na polisi katika kuhakikisha kuwa  sheria na kanuni za usafirishaji zilizowekwa zinazingatiwa.
Sumatra   imewataka wamiliki na  waendeshaji wa vyombo hivi kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani na kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kihuni na kulinda usalama wao wenyewe na abiria.

No comments:

Post a Comment