TANGAZO


Saturday, October 19, 2013

Meya Jerry Silaa na Kampeni kabambe za kuchangia madawati kupitia sanaa

DSC_0429

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari leo, asubuhi kuhusu kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’ kupitia wasanii mbalimbali wa kuchora nchini. Kulia kwake ni Msanii Robin Mtila na kushoto ni Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha na Mustafa Hassanali Mratibu wa Kampeni hiyo.
DSC_0446
Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha akizungumzia mchango wa hoteli yake katika kampeni ya Dawati ni Elimu yenye kauli mbiu ya "Kalisha mmoja boresha Elimu".
DSC_0457
Mchoraji Robin Mtila akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake ambapo ameelezea umuhimu wa sekta ya Elimu katika fani ya sanaa nchini.
DSC_0497
Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd Dhmy Jog akizungumza na waandishi wa habari baada ya kampuni yake kuchangia Tsh 10 milioni kwenye kampeni hiyo ya kuondoa tatizo la madawati katika shule za Msingi na Sekondari nchini.
DSC_0463
Baadhi wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha kubwa la Sanaa lenye lengo la kuchangia kampeni ya Dawati ni Elimu.
DSC_0466
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
DSC_0534
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Sanaa ya Uchoraji pamoja na baadhi ya wadhamini wa kampeni hiyo, Kampeni ya Dawati ni  Elimu yakusanya Tsh 1bilioni mpaka sasa lengo ni kufikia Tsh 4.98bilioni .atoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha la mwaka dawati ni elimu.

No comments:

Post a Comment