TANGAZO


Monday, October 14, 2013

Kilele cha Sherehe za Mwenge na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mkoani Iringa

Vijana wa Halaiki wakitoa burudani kwa kuimba nyimbo mbalimbali zinazohamasisha umoja wa taifa leo, wakati wa kilele cha mbio za mwenge wa uhuru katika viwanja vya Samora mjini Iringa.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2013, wakiingia katika Viwanja vya CCM, Samora mkoani Iringa leo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw. Juma Ali Simai akisoma risala ya ujumbe wa wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo mjini Iringa.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakimbiza mwenge wa Uhuru 2013 leo mjini Iringa.
Rais Jakaya Kikwete na mama Salma Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Fenella Mukangara (wa nne kutoka kushoto)
Wananchi wa mkoa wa Iringa na vijana wa halaiki wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge leo mkoani Iringa.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akifurahia jambo na wabunge wa Chama Demokrasia na Maendeleo wa Iringa (CHADEMA) akiwemo Mch. Peter Msigwa (wa pili kutoka kushoto)  leo wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Iringa.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere leo mjini Iringa wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2013.
Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa utajirishaji kutoka kwa Mkururugenzi wa Kampuni ya GODTEC alipotembelea banda lao wakati wa kilele cha mbio za Mwenge mkoani Iringa. 
Rais Jakaya Kikwete akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 Bw.Juma Ali Simai leo katika uwanja wa CCM Samora mjini Iringa. (Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)

No comments:

Post a Comment