TANGAZO


Monday, October 14, 2013

Uongozi wa Shirika la Changamoto za Milenia (Millenium Challange Corporation (MMC) wakutana na ujumbe wa Tanzania nchini Marekani

Ujumbe wa viongozi wa Tanzania, ukisikiliza uongozi wa Millenium Challenge Corporation (MCC), hawapo pichani, wakati walipokutana kwa majadiliano nchini Marekani jana. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, Balozi wa Tanzania nchi za Marekani na Mexico Liberata Mulamula, Waziri wa Fedha wa Dk. Wiliam Mgimwa, Waziri wa Fedha wa Zanzibar,  Yusuph Mzee na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamis Mussa. (Picha zote na Ingiahedi Mduma na Eva Valerian – Washington DC)
Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano na MCC mjini Washington. Kutoka kulia ni  Kamishna wa Fedha za Nje wa Jamhuri ya Muungano, Said Magonya, Kamishna wa Fedha za Nje Zanzibar, Bihindi Nassor, Naibu Ganana wa BOT, Dk. Natu Mwamba pamoja na Mkurugenzi wa Mipango Zanzibar.
Ujumbe wa Tanzania na Viongozi wa MCC katika majadiliano


WALATI mikutano ya mwaka ya Shirika la fedha la kimataifa na makundi ya benki ya Dunia ikiendelea hapa mjini Washington DC, Ujumbe kutoka Tanzania watumia nafasi hiyo kukutana na Uongozi wa Millenium Challenge Corporation (MCC), kwa madhumuni ya kujadili mafanikio yaliyopatikana kutokana na shirikahili la Marekani. MCC awamuya kwanza ilisaidia sana miradi mbalimabli Tanzania, ambapo walitoa dola milioni 698 ambayo ilielekezwa katika miradi ya barabara, umeme, maji pamoja na miradi ya barabara Zanzibar pamoja na uwanja wandege wa Mafia (Mafia Airport).
Akizungumza na vyombo vya Habari mjini hapa, Waziriwa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa, alisema kuwa “Miradi hiyo, yote ya MCC ya kwanza ili kwenda vizuri sana na tunamaliza nao mkataba tukiwa tumefanikiwa sana katika ujenzi wa miradi hiyo”.

Aidha, Mgimwa aliendelea kutoa ufafanuzi akisema kuwa “lengo kubwa la kukutana na Uongozi wa MCC ni kuangalia mafanikio yaliyo patikana katika miradi waliyoianzisha na ni nini tumejifunza kutoka katika hiyo miradi ili tuepuke matatizo katika miradi mingine inayofuata”.
Katika majadiliano hayo ujumbewa Tanzania ulipata fursa ya kuzungumzia miradi ya  MCC ya awamu ya pili ambapo, MCC wamekubali kuisaidia Tanzania kueneza umeme vijijini hasa vijiji vikubwa vinavyozalisha mazao kwa wingi na vijiji vyenye watu wengi pamoja na kujengabarabarakatikamaeneoyauzalishaji.


“Hiiitakuwanafasiya Tanzania kuwezakusaidiakuenezaumemevijijiniambapowananchiwetuwatapatanafasiyakutumiaumemehuokatikamiradimidogomidogona vile vile kwa ajili ya kuhakikisha kuwa miradi ya barabara hasa katika vijiji vinavyozalisha mazao wanaweza kupokea pembejeo na baada ya kuvuna kuweza kufikisha mazao yao kwa walaji.” AlifafanuaMgimwa.
Imetolewana:
Ingiahedi Mduma, Msemaji Mkuu, Wizara ya Fedha

No comments:

Post a Comment