Wengi wa wachimba migodi wa dhahabu ambao wamekuwa wakigoma tangu Jumanne nchini Afrika Kusini wamerejea kazini baada ya waajiri wao kukubali kuwapa nyongeza ya mishahara.
Kwa mujibu wa maafisa wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi, kampuni nne kati ya saba zimekubali kuwapa nyongeza wafanyakazi hao ambayo inaaminika kuwa asilimia 8.
Wachimba migodi walikuwa wametishia kuwa mgomo wa muda mrefu ungesababisha migodi kufungwa na maelfu ya watu kupoteza kazi zao, kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.Chama hicho kilikuwa kinataka 60%, wakati waajiri wao wakipendekeza kuwapa asilimia sita ikiwa sawa na kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo.
Wanasema kuwa bei ya kuzalisha madini hayo imepanda kwani wamelazimika kuchimba mita nyingi chini ya ardhi kupata madini hayo.
Kwa miaka mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote duniani uikiwa ni asilimia 68 mapema miaka ya sabini lakini mambo yamebedilika sasa ikiwa inazalisha tu asilimia sita ya dhahabu yote duniani, hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP
Chama cha wafanyakazi NUM kinawakilisha takriban asilimia 64 ya wachimbaji wa dhahabu kote nchini humo.
Mwaka jana wananchi wengi waliachwa vinywa wazi wakati polisi walipowaua wafanyakazi 34 wa migodi ya platinum wakati wa mgomo haramu ulioitishwa na chama hasimu cha wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment