TANGAZO


Sunday, September 15, 2013

Uongozi wa Shule ya Kimataifa ya Southern Highlands Mafinga, wawahakikishia wazazi ufaulu wa watoto wao


Mkurugenzi  mtendaji  wa  shule ya kimataifa  ya  Southern Highlands Mafinga  wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Bi. Mary A.Mungai akitoa  taarifa  ya mafanikio  ya  shule  hiyo jana  wakati  wa mahafali ya 13  ya  shule  hiyo. (Picha na Francis Godwin)

Na Francis Godwin,Iringa
WAKATI wanafunzi  wa darasa la  saba kote nchini  wakiendelea kusubiri matokeo ya mtihani   wa darasa la saba, uongozi  wa  shule ya  kimataifa  ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya  Mufindi mkoani hapa  umewahakikishia  wazazi kuwa wawe na uhakika mkubwa wa  watoto  wao  kufaulu mtihani  huo.

Mkurugenzi mtendaji  wa  shule hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata  kuwa afisa elimu wa  shule za msingi alitoa kauli  hiyo wakati  wa mahafali ya  13  ya darasa la  saba  shuleni hapo juzi.
Alisema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .
“Shule  yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”
Alisema katika  matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
“   Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai
Hata  hivyo  alisema kila wanafunzi wote  wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.
“Ninaamini wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, watafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari….. Sababu walikuwa wanapenda masomo na nidhamu yao ni nzuri.”
Kwa upande  wake mkurugenzi  wa bodi ya shule  hiyo Bw Omary Mahinya alisema kuwa katika moja ya vielelezo  kuwa shule  hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka  watoto wao hapo .
“Wahitimu toka shule yetu wamekuwa wakifanya vizuri katika Sekondari kidato cha IV na kidato cha VI popote walipo kwenda… hii inadhihirisha kuwa Southern Highlands School imewajengea msingi bora wa Elimu ambao ni TUNU ya kujivunia sana. 
Aidha  alisema  kuwa lengo la uongozi wa shule hiyo ni kuhakikisha kuwa Southern Highlands School inakuwa mfano bora na kioo kwa jamii inayotuzunguka kwa kuweka mazingira bora ya kuishi.

No comments:

Post a Comment