TANGAZO


Wednesday, September 18, 2013

Shirika la Taifa la Maendeleo lakutana na waandishi wa habari

IMG_7012
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa Serikali  kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka za chuma, mara uzalishaji wa madini hayo, utakapoanza mwaka 2018/19 chini ya Kampuni ya Tanzania China Mineral Resources Limited (TCIMRL) na kuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa madini hayo barani Afrika, aliyaeleza hayo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Fatma Salum. (Picha zote na Hassan Silayo - Maelezo)
IMG_7018
Mkuu wa Kitengo cha Viwanda vya Kemikali toka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abdallah Mandwanga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu faida za uzalishaji wa madini ya Titanium takribani tani 175,400 na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam leo.
IMG_7029
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba, akiwaonesha waandishi wa habari picha ya mchoro wa kiwanda cha chuma cha Liganga, wakati wa mkutano na waandishi, uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari, Fatma Salum. 

No comments:

Post a Comment