Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akielezea jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Catherine Sungura.
Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Catherine Sungura.
Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Catherine Sungura.
Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiongea nao kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Catherine Sungura.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini.
Mratibu wa Taifa, Mpango wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, Dk. Upendo Mwingira (katikati), kutoa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mpango wa Serikali juu ya kudhibiti magonjwa hayo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Catherine Sungura.
SERA ya afya ina lengo la kuinua hali ya maisha kwa
wananchi wote mahali popote walipo ikiwa mjini au vijijini kwa kupunguza
maradhi na vifo kwa wananchi na kuongeza umri wa maisha yao kwa kuwa na afya
thabiti kimwili, kiakili na kijamii. Vilevile ieleweke kwamba afya bora ni
rasilimali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kiakili.
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
imejikita katika kuimarisha, kuboresha
na kusambaza huduma za afya na ustawi wa jamii nchini, kwa kuzingatia Mpango wa
Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM-2007-2017),imejikita katika kudhibiti magonjwa
yasiyopewa kipaumbele.
Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni magonjwa ambayo yanaathiri
jamii ya watu hususani wenye kipato cha
chini wanaoishi katika maeneo duni, maeneo ambayo hata upatikanaji wa huduma za afya ni mgumu.
Magonjwa hayo ni pamoja na Matende na mabusha, Usubi, Trakoma,
Kichocho, Minyoo ya tumbo,Homa ya malale,Kichaa cha mbwa,tauni,Tegu na
mengineyo.Maambukizi ya Magonjwa haya yanatokana na kuenezwa
na wadudu kama vile mbu, nzi na konokono. Udhibiti wa magonjwa haya
unaelekezwa kwenye kinga tiba,usafi binafsi wa mazingira na udhibiti wa wadudu
waenezao magonjwa hayo.
Athari za magonjwa
haya yasipotibiwa mapema ni
pamoja na saratani ya kibofu cha mkojo
na ini,upofu,utumbo kujifunga na dalili za kifafa.Magonjwa haya husabababisha
pia ulemavu wa kudumu hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi wetu kushiriki
katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi.
Magonjwa haya huathiri pia watoto na hivyo
kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni hatimaye maendeleo yao katika
masomo kuathirika. Magonjwa haya husababisha
usumbufu mkubwa kwa waathirika wake na
yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili
kwa gharama kubwa mno. Pamoja na athari zote hizo, waathirika wa magonjwa
haya wakabiliwa na unyapaa katika jamii.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepiga hatua kubwa
katika udhibiti wa magonjwa hayo kwa
kuimarisha, kuboresha na kusambaza huduma za Mpango wa Taifa wa kudhibiti
Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kwa jamii zilizoathirika nchini. Katika mwaka
2012/2013, wizara kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa
hayapewi Kipaumbele imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:
·
Kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa Magonjwa yasiyopewa
Kipaumbele (2012-2017).
·
Kuongeza idadi ya wilaya zinazotekeleza
mpango huu kutoka 76 mwaka 2011 hadi
halmashauri 93 kati ya 155 yaani asilimia 60% halmashauri zote kwa nchi nzima
·
Kutibu na kukinga watu
milioni 15.4 kwa dozi million 36 za dawa za Mectizan, Albendazole,
praziquantel na Zithromax.
·
Kufanya Tathminini ya awali ya ugonjwa wa Trachoma katika wilaya 9. Matokeo
yanaonyesha Wilaya 10 zilizofanyiwa tathmini hiyo hazihitaji kinga tiba i.e MDA
·
Uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa dawa katika jiji la Dar (kwa jamii) pamoja na
Mwanza ( mashuleni).
Kwa kiasi kikubwa serikali imejitahidi kuboresha huduma
za udhibiti wa magonjwa hawa kwa kusambaza dawa za kingatiba za magonjwa haya
katika wilaya 97 kupitia Bohari kuu ya Madawa,kuwa na waratibu wa Mpango huu
katika ngazi za Mkoa na wilaya.Waratibu hawa wanapatiwa Mafunzo na maelekezo ya
utekelezaji wa mpango kila mwaka.Utekelezaji wa Mpango huu unafanyika katika ngazi ya
wilaya na hivyo Halmashauri zote zilizoathirika zimeelekezwa kutenga rasilimali katika mipango yao ya Afya
kupitia Muongozo wa CCHP.
Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kumeza dawa
hizi za Kingatiba kama wanavyoelekezwa na wataalam wakati wa Kampeni
husika.Dawa hizi zimethibitishwa na shirika la afya duniani pamoja na mamlaka
ya Chakula na dawa nchini kuwa ni salama na hazina Madhara yeyote.
No comments:
Post a Comment