TANGAZO


Saturday, September 14, 2013

Ligi Kuu ya Vodacom, Simba yaichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Mtibwa Sugar ya Morogoro wakati zilipochuana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Simba imeshinda mabao 2-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Mtibwa Sugar ya Morogoro wakati zilipochuana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. 
Wachezaji Hassan Ramadhan (kushoto) wa Mtibwa Sugar na Haruna Chanongo wa Simba, wakiwania mpira wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.Simba imeshinda mabao 2-0.
Hassan Ramadhan (kushoto) wa Mtibwa Sugar na Haruna Chanongo wa Simba, wakiwania mpira huo, wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa.  
Hassan Ramadhan  wa Mtibwa Sugar na Haruna Chanongo wa Simba, wakiwania mpira huo.  
Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar akijaribu kumhadaa Haruna Chanongo wa Simba katika mchezo huo. 
Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar akiendelea kumhadaa Haruna Chanongo wa
Simba katika mchezo huo.  
Issa Rashid wa Simba, akijaribu kumtoka Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar, katika mchezo huo.
Issa Rashid wa Simba, akimtoka Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar. 
Issa Rashid wa Simba, akipiga mpira huo mbele ya Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar.
Beki wa Mtibwa, Hassan Ramadhan, akiondoa mpira miguuni mwa Issa Ramadhan wa Simba wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 2-0. 
Golikipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif, akiruka kouondoa mpira wa juu ambao hata hivyo ulimpita na kumfikia Henry Joseph aliyeruka na kuupiga kichwa na kisha kuwa bao la kwanza kwa timu yake ya Simba.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Henry Joseph (14) dhidi ya Mtibwa Sugar.
Haruna Chanongo wa Simba akitumia ubavu kumzuia Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo. 
Haruna Chanongo wa Simba akimtoka Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar.
Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar, akijaribu kuutoa mpira miguuni mwa Haruna Chanongo wa Simba. 
 Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo.
Hassan Ramadhan wa Mtibwa Sugar na Haruna Chanongo wa Simba, wakiruka juu kuwania mpira huo. 

TIMU ya soka ya Simba imefanikiwa kuendeleza wimbi lake la ushindi baada ya leo kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabingwa hao wa zamani walilazimika kutumia kipindi cha pili vizuri ili kujihakikishia ushindi huo.

Mtibwa walionekana kuanza pambano hilo kwa kasi na kuonesha uhai katika kushambulia kuliko Simba, ambao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.

Iliwachukua dakiika 15 kwa Mtibwa kuonesha kuwa wamefuata pointi tatu Dar es Salaam kwani winga mshambuliaji, Vicent Barnabas angeweza kuiandikia Mtibwa bao la kuongoza.

Barnabas, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, alishindwa kupiga vizuri mpira wa mwisho katika piga nikupige langoni mwa Simba.

Kasi ilizidi na dakika ya 34, kiungo Shaaban Kisiga alishindwa tena kuipa bao Mtibwa, baada ya kuchelewa kuunganisha pasi ya Ally Shomari.

Mtibwa walifanikiwa kuishambulia Simba mfululizo dakika zaidi ya 20, ambapo umakini wa safu ya ulinzi uliwaokoa mabingwa hao wa zamani kuruhusu bao la mapema.

Simba walizinduka dakika ya 38 na kufanya shambulizi la kushitukiza, lakini krosi ya beki Nassor Masoud 'Chollo' ilishindwa kuunganishwa na mshambuliaji, Amissi Tambwe, ambaye shuti lake hafifu lilimgonga beki wa Mtibwa mkononi.

Tukio hilo la kushikwa kwa mpira huo ndani ya eneo la hatari liliwafanya wachezaji wa Simba kumzonga mwamuzi wa mchezo huo wakidai penalti, lakini hata hivyo madai yao hayakusikilizwa.

Mtibwa Sugar iliamua kuongeza nguvu kwa kumuingiza mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, ambaye alichukua nafasi ya Juma Liuzio.

Kuingia kwa Mgosi kulionesha matumaini na mshambuliaji huyo kufanya kazi ya ziada baada ya kumpiga chenga safi Issa Rashid na kujaza krosi, lakini kipa wa Simba, Abel Dhaira alifanikiwa kutokea na kuudaka mpira huo.

Simba iliona udhaifu katika safu ya kiungo, ambapo kocha Abdallah Kibadeni aliamua kumuingiza kiungo mkongwe Henry Joseph, akichukua nafasi ya Said Hamisi.

Barnabas, ambaye katika mchezo huo alionesha uhai mkubwa, angeweza kuipa Mtibwa bao, baada ya kufanikiwa kupiga mkwaju hatari nje ya 18, lakini kipa, Dhaira, aliuona na kuudaka dakika ya 57.

Kuingia kwa Henry kulikuwa mafanikio kwa Simba, kwani kiungo huyo aliiandikia timu yake ba la kuongoza kwa kichwa dakika ya 67.

Kipa wa Mtibwa, Hassan Sharrif alipangua vizuri mpira wa kona ya Haruna Chanongo, ambao ulirudi kwa Tambwe aliyeumimina vizuri kwa mfungaji.

Bao hilo liliwaamsha Simba, ambao walikuwa wameelemewa katika kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizi ya kila mara langoni kwa Mtibwa.

Betram Mombeki aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Twaha Ibrahim, alifanikiwa kuhitimisha ushindi wa Simba kwa kufunga bao la pili kwa shuti kali akitumia pasi ya Ramadhani Singano dakika ya 89.

Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi saba, baada ya kwenda sare mchezo mmoja dhidi ya Rhino Rangers, ushindi dhidi ya JKT Oljoro na kisha leo kuichapa Mtibwa Sugar 2-0.

No comments:

Post a Comment