TANGAZO


Friday, August 16, 2013

Waziri Lwenge akagua nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dar es Salaam

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga (kulia), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi,  Mhandisi 
Geryson Lwenge, ramani ya nyumba zinazojengwa 
na TBA maeneo ya Bunju B ambazo watauziwa 
watumishi wa Serikali  wakati waziri huyo 
alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja ya 
kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba hizo,  
Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa 
Mradi huo, Wilfred Dungamu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga (kulia), akitoa taarifa fupi ya ujenzi huo mbele ya Naibu Waziri Lwenge (katikati). Kushoto ni Mkurugenzi wa Majengo wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Optatus Kanyesi
Naibu Waziri wa Ujenzi,  Mhandisi Geryson Lwenge, akitoa taarifa ya ujenzi huo. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga na 
Mkurugenzi wa Majengo wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Optatus Kanyesi.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa maeneo ya Bunju B.
  Naibu Waziri wa Ujenzi,  Mhandisi Geryson Lwenge (kushoto), akimuelekeza jamboOfisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga (katikati)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Elius Mwakalinga (kulia), akimuelekeza jambo Waziri Lwenge wakati akikagua nyumba hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Greyson Lwenge (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari eneo la mradi. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kushoto), akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Greyson Lwenge (wa pili kushoto), wakati wa ukaguzi wa mradi huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Majengo wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Optatus Kanyesi. Wengine ni maofisa kutoka wizara hiyo, TBA na wajenzi wa mradi huo.
Nyumba zinazojengwa maeneo ya Mbezi Beach. 
Waziri Lwenge akitoka kukagua nyumba zinazojengwa Mbezi Beach.
Waziri Lwenge(katikati) na Mtendaji Mkuu wa TBA (kushoto) wakiongoza maofisa wengine wakati wa ukaguzi wa nyumba hizo. (Picha zote na habari na www.mwaibale.blogspot.com)


Na Dotto Mwaibale
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA), imetumia zaidi ya sh.bilioni 4.3 kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi za gharama nafuu watakazouziwa watumishi wa serikali.

Nyumba hizo zinajengwa maeneo ya Bunju B na Mbezi katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuwanufaisha wafanyakazi hao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya siku moja ya kukagua nyumba hizo iliyofanyika leo Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Greyson Lwenge alisema ujenzi wa nyumba hizo ni mpango wa serikali kuhakikisha inawapatia watumishi wake makazi bora na ya bei nafuu.

" Ujenzi wa nyumba hizi ni mpango wa serikali wa kujenga nyumba za bei nafuu ambazo zitauzwa kwa watumishi wake" alisema Lwenge.

Alisema kwa awamu ya kwanza zaidi ya sh.bilioni 2.2 zilitumika na kwa awamu yapili zitatumika sh.bilioni 2.3 na fedha hizo ni mkopo kutoka benki kuu.

Aliongeza kuwa nyumba hizo zikikamilika zitauzwa sh.milioni 30 kwa nyumba moja bei ambayo ni  ya chini tofauti na ile ambayo ingetozwa na wakandarasi ambao wangepewa mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Mhandisi Elius Mwakalinga alisema kupitia mradi huo nyumba 10,000 zitajengwa kwa nchi nzima na kwa Dar es Salaam nyumba 1400 zitajengwa.

Alisema nyumba zinazojengwa hivi sasa katika mradi wa Bunju B ni 155 na zinatarajiwa kukamilika novemba mwaka huu.

Mratibu wa Mradi huo Hamphrey Sillo alisema katika awamu ya kwanza wa ujenzi huo walikumbana na changamoto kadhaa zikiwepo kuongeza kwa kiasi cha sh.milioni 700 katika fedha zilizo kadiriwa.

Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya watu kuibuka na kudai maeneo zilipojengwa nyumba hizo ni mali yao hivyo kujikuta wakiingia hasara ya zaidi ya sh. milioni 35.8 za vifaa na gharama walizotumia kujengea nyumba hizo zilizofikia hatua ya msingi.

"Changamoto nyingine ni hali ya hewa kutokana na mvua nyingi zilizosababisha ujenzi kusimama, kukosekana kwa wataalamu, vifaa vya ujenzi na fedha za kuendesha kwa mradi huo" alisema Sillo.

No comments:

Post a Comment