TANGAZO


Saturday, August 17, 2013

Waandamanaji Misri watolewa msikitini

Majeshi ya usalama ya Misri yameondoa watu katika msikiti mmoja mjini Cairo, baada ya mvutano wa muda mrefu na wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood. Waandamanaji hao waliokuwa ndani wametolewa nje ya msikiti, na wengi wamekamatwa, kwa mujibu wa majeshi ya usalama.
Misri
Purukushani nje ya msikiti wa al-Fath mjini Cairo
Makabiliano katika msikiti wa al-Fath yaliendelea kwa siku nzima, na hata majibizano ya risasi kutokea kati ya majeshi ya usalama wa waandamanaji.
Wakati huohuo Waziri Mkuu wa mpito amependekeza kuvunnja chama cha Brotherhood kwa njia halali. Chama hicho kinamuunga mkono Rais aliyetolewa madarakani Mohammed Morsi, na kinataka arejeshwe madarakani.
Licha ya kuhusishwa kwa karibu na serikali ya Bw Morsi, chama cha Brotherhood ni taasisi ambayo imepigwa marufuku. Kilivunjwa rasmi na watawala wa jeshi la Misri mwaka 1954, lakini hivi karibuni kimejiandikisha kama chama kisicho cha kiserikali.

No comments:

Post a Comment