TANGAZO


Monday, August 26, 2013

Rais Jakaya Kikwete amwapisha Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Msajili mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.
Msajili mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akisaini hati za kiapo, mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete Ikulu, akisaini hati za kumwapisha Msajili mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kulia), jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kumwapisha Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Msajili mpya wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi Ikulu, jijini Dar es Salaam mara baada ya kumwapisha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na Msajili wa Vyama vya Siasa mstaafu, John Tendwa baada ya kumwapisha Jaji Mutungi, Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja naMsajili mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Ikulu)


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumatatu, Agosti 26, 2013, amemwapisha Jaji Francis Sales Katabazi Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa mpya.

Jaji Mutungi anachukua nafasi ya Bwana John Tendwa ambaye amestaafu kutoka Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Sherehe za kumwapisha Jaji Mutungi zilizofanyika Ikulu, Dar Es Salaam zimehudhuriwa pia na Jaji  Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi Mheshimiwa Fakhi Abdallah Rheno Jundu pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment