Watu saba wameuawa mjini Cairo usiku wa kuamkia leo kufuatia makabiliano makali kati ta wanajeshi wa serikali na wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi.
Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya na kuwasukuma nyuma waandamanaji hao ambao walikuwa wakiwarushia mawe huku wakiwa wamefunga barabara kuu inayoelekea kati kati mwa mji mkuu.
Ghasia hizo zimetokea huku naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, William Burns akiwa ziarani nchini humo.
Waziri huyo amesema taifa hilo limepewa nafasi ya pili kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Bwana Burn alifanya mashauriano na viongozi wa serikali ya mpito ya nchi hiyo, lakini viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood, walisusia mkutano huo.
Awali mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa Cairo na kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi.
Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo.
Makabiliano yalifanyika baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi.
Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi nchini, mjumbe huyo, William Burns, amesema Misri imepewa nafasi ya pili kufuatia kupinduliwa na jeshi Mohammed Morsi.
Alikutana na serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini lakini Muslim Brotherhood, inasema haina mpango wa kukutana naye. Naibu rais wa tawi la kisiasa la chama cha Morsi, Muslim Brotherhood,Essam el-Erian, ametoa wito wa utulivu.
No comments:
Post a Comment