TANGAZO


Monday, July 29, 2013

Wafuasi wa Morsi waendelea kuandamana


Mjumbe wa Ulaya Catherene Ashton yuko Misri kujaribu kutuliza hali
Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi wamepanga maandamano zaidi kuelekea kambi za kijeshi. Pia wameitisha maandamano makubwa hapo kesho Jumanne.
Haya yanajiri huku, Mjumbe wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya akiwa mjini Cairo kwa mazungumzo ya kumaliza taharuki zinazoendelea kufuatia mauaji ya zaidi ya waandamanji 70 wengi wakiwa wafuasi wa Muslim Brothehood.
Maelfu ya wafuasi wa Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi nje ya msikiti mashariki mwa Cairo kwa majuma kadhaa sasa na wanapanga kuendelea na maandamano yao usiku kucha.
Waandamanji hao wameitisha maandamano makubwa hapo kesho jumanne kuelekea katika kambi kuu ya jeshi.
Wanajeshi waliomuondoa madarakani Bw. Morsi wameonya waandamanaji dhidi ya kuhatarisha usalama wa kitaifa.
Wanajeshi wamesema yeyote atakayekiuka amri atakabiliwa vilivyo.Tayari viongozi wengi wa Muslim Brotherhood wamekamatwa au wamewekewa vibali vya kukamatwa.
Huku haya yakiarifiwa Mjumbe wa muungano wa Ulaya Chatherene Ashton anakutana na pande zote za kisiasa nchini Misri. Hata hivyo hali ya sasa ni dhahiri kwamba hakuna ushawishi wowote wa kimataifa utakaobadilisha mzozo wa sasa.

No comments:

Post a Comment