TANGAZO


Thursday, July 11, 2013

Taarifa: MAJUKUMU YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI BAADA YA UGATUAJI WA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA SHULE ZA SEKONDARI

Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayeshughulikia vitengo vya mawasiliano serikalini, Zamaradi Kawawa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, kuzungumzia kuhusu majukumu ya wizara hiyo, baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa Shule za Sekondari nchini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu majukumu ya wizara hiyo baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa Shule za Sekondari nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayeshughulikia vitengo vya mawasiliano serikalini, Zamaradi Kawawa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu majukumu ya wizara hiyo baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa Shule za Sekondari nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayeshughulikia vitengo vya mawasiliano serikalini, Zamaradi Kawawa.
Waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo, wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu majukumu ya wizara hiyo baada ya ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa Shule za Sekondari nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, anayeshughulikia vitengo vya mawasiliano serikalini, Zamaradi Kawawa.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, Dar es Salaam leo.

KAMA mnavyofahamu Ugatuaji (decentralization)  wa usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kwenda katika ngazi ya Halmashauri ulifuatia ongezeko kubwa la shule za sekondari na wanafunzi ambalo lilisababisha mahitaji ya walimu na huduma za uendeshaji wa shule kuongezeka. Hali hii ilisababisha usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi moja kwa moja kuwa mgumu na hivyo kuchelewesha utoaji wa huduma. Ili kupata ufanisi zaidi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnamo tarehe 12/02/2008 alitoa tamko la  kusogeza huduma za uendeshaji na usimamizi wa shule za sekondari kwenye ngazi ya Halmashauri.
Ugatuaji wa uendeshaji wa masuala ya elimu kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa ulianza miaka ya 1970 ilipogatuliwa elimu ya Msingi. Kufuatia ugatuaji wa usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kwenda katika ngazi ya Halmashauri uliofanywa na Serikali mwaka 2008/2009, majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yamegawanywa kati ya wizara hizo mbili kwa kuzingatia majukumu ya msingi yanayohusisha elimu ya msingi na sekondari.
Hivyo, kuhusu masuala ya elimu ya msingi na sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ina majukumu ya kusimamia masuala ya sera, viwango, utafiti, ufuatiliaji na tathmini.
Aidha, Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi ina majukumu ya kusimamia utekelezaji na utoaji wa elimu kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini, pamoja na kufanya mapitio, kuandaa na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sera, mipango, sheria na kanuni za elimu zilizopo kulingana na mabadiliko ya dhima na dira ya serikali; na kuandaa Mikakati ya utekelezaji wake. Halikadhalika, Wizara hii ndiye msimamizi Mkuu wa Masuala ya taaluma katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
Pia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaendelea kusimamia na kuendesha vyuo vya ualimu na shule za Mazoezi, msingi na sekondari zilizopo katika vyuo vya ualimu vya serikali.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inasimamia uendeshaji wa shule za msingi na sekondari  ambapo Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji zinawajibika katika kutekeleza jukumu hili. Aidha, Serikali imeanzisha Idara ya Elimu ya Sekondari katika kila Halmashauri ambapo mkuu wake wa Idara ni Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri mwenye jukumu la kusimamia uendeshaji wa shule za sekondari.
Hivyo basi, wadau wa elimu wanatakiwa kuelewa  mgawanyo huu wa majukumu baada ya ugatuaji wa usimamizi na Uendeshaji wa shule za sekondari ambapo masuala ya uhamisho wa walimu na wanafunzi pia malipo ya stahiki za walimu na watumishi wengine walioko shuleni yanafanywa na  Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Masuala yote yanayohusu utendaji wa shule za msingi na sekondari yanasimamiwa moja kwa moja na Halmashauri ili kuongeza tija na uwajibikaji.
Imetolewa na:
Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
11/07/2013

No comments:

Post a Comment