TANGAZO


Thursday, July 18, 2013

Serikali kuondoa vibali vya upatikanaji wa Wakandarasi

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Maji, Nurdin Ndimbe akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji vijijini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini kutoka wizara hiyo, Mhandisi Karangi Bwire. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)

Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Dawasa, Boniface Kasiga akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji toka Wizara ya Maji akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu taratibu za wananchi kufuata wakati wa uchimbaji wa visima. 




Hassan Silayo-Maelezo
SERIKALI kupitia wizara ya maji imepania kuondoa vibali vinavyotolewa na Wizara hiyo katika kupata Wakandarasi, Wataalam, Washauri na kupitisha taarifa za usanifu ili kutekeleza kwa haraka miradi mbalimbali ya maji nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Nurdin Ndimbe kutoka Wizara ya Maji wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

ìkatika kuhakikisha serikali kupitia wizara yetu inatekeleza miradi mbalimbali ya maji vijijini tumeamua Kuondoa vibali vinavyotolewa na Wizara katika kupata Wakandarasi, Wataalam Washauri na kupitisha taarifa za usanifu  kulingana na waraka uliotoka tarehe  Juni 7 mwaka huuî alisema Nurdin.

Aidha Nurdin alisema ili kuboresha mfumo wa ufuatiliaji wizara imeunda chombo cha ufuatiliaji kinachoitwa Ministerial Delivery Bureau kikiwa na dhumuni la kuboresha na kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na Wizara hiyo inatekelezeka ndani ya mda uliopangwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali Maji kutoka Wizara hiyo Naumia Rupime amewataka wananchi kuacha kuchimba visima kiholela badala yake wafuate taratibu  na sheria zilizowekwa ili kuondoa kero mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

ìwananchi wamekuwa wakichimba visima kiholela na kuuza maji bila kufuata taratibu ikiwa ni kwenda kwa msajili wa mabonde katika eneo husika au bila ya kupeleka sampuli ya maji yaliyochimbwa katika Maabara ili kuthibitisha usalama wa maji hayo. alisema Naumia.

Jumla ya miradi ya maji kwenye vijiji 682 ikiwa ni wastani wa vijiji 5 kwa kila Halmashauri vipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji. Ifikapo mwezi Septemba 2013 ujenzi wa miundombinu ya maji utakuwa umekamilika  ambapo jumla ya watu milion 1.7 wanatarajiwa kupata huduma ya maji.

No comments:

Post a Comment