Mjukuu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ambaye yuko katika hali mahututi katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, amesema kuwa amehuzunishwa sana na mzozo unaokumbwa familia yake.
Familia ya Mandela imekuwa ikilumbana kuhusu kurejeshwa kwa mabaki ya watoto watatu wa Mandela katika makaburi yao ya zamani.
Akizungumza na BBC kabla ya maadhimisho ya miaka 95 tangu kuzaliwa kwa rais huyo kwa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Ndileka Mandela amesema familia yake imekuwa na kibarua kigumu kukabiliana na hali ya afya ya Mzee Mandela.
Mzozo huo umekuwa kati ya wanachama kumi na sita wa familia na Mandela akiwemo mke wake, Graca Machel na mjukuu wa kwanza wa kiume wa Mandela ambaye pia ni kiongozi wa koo hiyo, Mandla Mandela.
Familia hiyo ilikwenda mahakamani, tarehe tatu Julai mwaka huu, kushininiza mabaki ya watoto hao watatu wa Mandela kufukuliwa na kurejeshwa katika makaburi ya ya zamani katika eneo la Qunu, mkoa wa Mashariki wa Cape.
Mandla alikuwa amefukua mabaki ya watatu hao ya kuyazika upya katika eneo la Mvezo bila idhini au kushauriana na wanachama wengine wa familia ya Mandela kutoka koo la Aba Thembu.
Kwenye nyaraka iliyowasilishwa mahakamani, inadaiwa Mandla alihamishwa mabaki hayo ili kuhakikisha kuwa Mandela amezikwa katika eneo hilo la Mvezo.
Mabaki hayo yaliyozikwa tena katika eneo la Qunu ni ya Makgatho Mandela ambaye ni babake Mandla ambaye aliaga dunia mwaka wa 2005 kutokana na maambukizi yanayohusiana na virusi vya ukimwi, Thembekile, ambaye aliaga dunia kwenye ajali ya barabarani mwaka wa sitini na tisa na babake Ndileka na Makaziwe mwanawe wa kike kwa kwanza wa Mandela ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miezi tisa pekee.
Ndileka amesema mzozo kuhusu makaburi ni jambo la kusitisha lakini hautasababisha familia hiyo kusambaratika.
No comments:
Post a Comment