Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, alimkabidhi kibali cha ujenzi wa kiwanja cha Kidongo Chekundu, Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha michezo cha Symbion, Ulrik Muller, kitakachojengwa kwa ufadhili wa timu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni hiyo ya kufua umeme, Dar es Salaam leo. Wafadhili hao, wamepatikana kutokana na juhudi za Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (kushoto).
Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha michezo cha Symbion, Ulrik Muller, akimkabidhi jezi ya timu ya Sunderland Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu wakati wa hafla ya kukabidhi kibali cha ujenzi wa Uwanja wa Kituo cha Michezo cha Symbion katika kiwanja cha Kidongo Chekundu, Dar es Salaam leo. Ujenzi huo umefadhiliwa na Kampuni hiyo ya kufua umeme pamoja na timu ya Sunderland ya Uingereza kutokana na juhudi za Mbunge huyo wa Ilala.
Huu ndiyo mchoro wa kiwanja cha Kituo hicho cha michezo, kilichokabidhiwa kibali cha ujenzi wake na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, Dar es Salaam leo. Wafadhili hao, wamepatikana kutokana na juhudi za Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, akizungumza katika hafla ya kukabidhi kibali hicho cha ujenzi wa Uwanja wa kituo hicho.
KAMPUNI ya Uzalishaji umeme ya Symbion kwa kushirikiana na Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza leo, imekabidhiwa kibali cha kuanza ujenzi wa kiwanja cha michezo ya vijana 'academy' kilichopo kidongo chekundu jijini Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa alimkabidhi kibali hicho Mkurugenzi wa Mradi huo, Ulrik Muller wa Kampuni ya Symbion ambaye alisema ujenzi huo utaanza hivi karibuni.
Akizungumza na bayana.blogspot, Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, ambaye ndiye aliyefanya juhudi za kuwatafuta wafadhili hao, alisema kuwa anaishukuru timu ya Sunderland na Kampuni ya Symbion ambao kwa pamoja wameamua kulisaidia jimbo lake.
Mkurugenzi wa mradi huo 'Muller' amesema Uwanja huo, utakuwa na viwanja vitatu ndani yake ambapo kutakuwa na viwanja vya michezo tofautitofauti.
No comments:
Post a Comment