TANGAZO


Sunday, July 21, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal afanya ziara ya kukagua shughuli za usafi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kulia), akisalimiana na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipowasili viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea ripoti ya hali ya usafi na mazingira jijini leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia viongozi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kusomewa ripoti ya hali ya usafi na mazingira ya jiji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto), kabla ya kuanza safari yake ya kukagua shughuli za usafi jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa katika Ofisi yake, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa.
Baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Ilala, wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati alipokuwa akiwahutubia viongozi wa jiji kabla ya kuanza safari yake mkoani Dar es Salaam kukagua shughuli za usafi jijini leo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akipewa maelezo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa (kulia), kuhusu hali ya usafi kwenye Kituo Kikuu cha daladala cha Mbagala, wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za usafi jijini Dar es Salaam leo.Mkuu wa Polisi (OCD) wa Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala, Jonathan Mshana, akitoa taarifa ya hali ya ulinzi shirikishi kwa Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, alipofika Kituo Kikuu cha Daladala, Mbagala Rangitatu leo katika ziara yake ya kukagua hali ya usafi jijini,
Vijana wa Polisi Jamii (Wana Ulinzi Shirikishi), wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia alipofika kituoni hapo katika ziara yake hiyo leo.
Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi pamoja na wafanyabiashara wa daladala, vioski na Polisi Jamii alipofika kituo cha Daladala cha Mbagala Rangi Tatu leo asubuhi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akipatiwa maelezo na mmoja wa viongozi wa Kituo cha Daladala cha Mbagala, Siaga Kiboko (kushoto), wakati akitembelea kituo hicho kuangalia hali ya usafi.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na akinamama wa mama ntilie kituoni hapo. 
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akipewa maelezo na Waziri wa Nchi, katika Ofisi yake, Mazingira, Dk. Terezya Huvisa (kulia), kuhusu hali ya usafi kwenye Kituo Kikuu cha daladala cha Mbagala, wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua shughuli za usafi jijini Dar es Salaam leo
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Sarah Yohana (kulia), akimpatia maelezo kuhusu dampo la Pugu Kinyerezi Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), wakati alipotembelea dampo hilo, kuangalia hali ya utupaji taka. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa, Said Fundi, akimpatia maelezo ya usafi wa mitaro na maeneo mengine ya Kata hiyo, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), alipofika maeneo hayo katika ziara yake hiyo leo.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (wapili kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiangalia mtaro wa maji taka, maeneo ya Majumbasita, Barabara ya Pugu leo.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akikagua Soko la Buguruni wakati wa ziara yake hiyo jijini leo. Wapili kushoto ni Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Buguruni, Said Habibu (kushoto), akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), kuhusu masuala ya usafi na usafishaji wa soko hilo wakati wa ziara hiyo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Jackson Midalla (kulia), akimueleza Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal hali ya utunzaji wa mabwawa ya maji taka, wakati alipotembelea mabwawa hayo, Buguruni Spenco wakati wa ziara yake hiyo leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Sadiki na wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Terezya Huvisa.

No comments:

Post a Comment