Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na mdau wa lugha ya Kwaswahili, Mohammed Seif Khatibu akitoa maoni kueleza umuhimu wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za lugha ya Kiswahili katika mkutano wa wadau wa Kiswahili uliofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana Alhamisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mwakumbusho ya Taifa, Eliwasa Maro akizungumzia umuhimu wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za lugha ya Kiswahil.
Mwanazuoni na
Mtaalamu wa Lugha ya Kiswahili, Profesa Mugyabuso Mulokozi naye alikuwa mmoja
wa waliotoa maoni yao juu ya kuanzishwa kituo hicho.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Manedeleo ya Utamaduni Lilian Bereko akichangia jambo katika
mkutano wa kujadili kituo hicho.Kuanzia kulia Aliyekuwa Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na mdau wa lugha ya Kwaswahili, Dk. Mohammed Seif Khatibu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuanzisha Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Lugha ya Kiswahili Boniface Sanjura , Mkurugenzi Mkuu wa Mwakumbusho ya Taifa, Eliwasa Maro, Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania, Monday Lukwepa na Afisa Utamaduni Habibu Msami waki, wakiwa wamesimama kumkumbuka marehemu Sijiana Saleh Mandevu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chama cha Ushairi Tanzania (UKUTA), aliyefariki Mei mwaka huu kwenye mkutano huo.
Mtaalamu wa Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Aldin Mutembei akitoa maoni na kueleza umuhimu wa kituo hicho.Pia ameteuliwa kuandika mapendekezo juu ya kuanzishwa kituo hicho.
Wadau wa Kiswahili wakifuatia kwa makini mkutano wa kujadili Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za lugha ya Kiswahili.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Kuanzisha Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Lugha ya Kiswahili
Boniface Sanjura wa kwanza kushoto, akitoa maelezo kuhusu chumba kilichopo
kwenye Makumbusho ya Taifa kilichotolewa kwa lengo la kuanzisha Kituo cha
Kuifadhi Kumbukumbu za lugha ya Kiswahili. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO)
Na Hussein Makame,
MAELEZO
MWANYEKITI wa
Kamati ya Kuanzisha Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu za Lugha ya Kiswahili
Boniface Sanjura amewataka wadau
wa Kiswahili nchini kuwajibika katika kulinda kumbukumbu muhimu za Taifa
ikiwemo lugha ya Kiswahili.
Mwenyekiti Sanjura
alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam, wakati akiwatambulisha wadau wa
Kiswahili chumba kilichotolewa na Kituo cha Makumbusho kwa lengo la kuhifadhia
kumbukumbu za Kiswahili.
Alisema kituo
hicho kitatumika kuhifadhi kumbukumbu muhimu za lugha ya Kiswahili ikiwemo
vitabu, machapicho, picha za magwiji wa lugha hiyo na kazi za Kiswahili na
kuwaomba wadau washiriki katika kufanikisha lengo kwa kukusanya kumbukumbu
hizo.
Akizungumza kuhusu
kituo hicho, mwenyekiti Sanjura alisema kituo hicho kitatumiwa wananchi ikiwemo
wanafunzi kutoka ngazi zote za elimu kupata taarifa muhimu kuhusu lugha ya
Kiswahili.
Naye Mkurugenzi Mkuu
wa Mwakumbusho ya Taifa, Eliwasa Maro alisema makumbusho yaliamua kutoa eneo hilo kwa ajili
ya kituo hicho ili kuzifanya kumbukumbu muhimu za lugha ya Kiswahili kunufaisha
kizazi cha sasa na kijacho ikiwemoku kuwasaidia watafiti na wanafunzi.
Aliwaomba wadau wa
Kiswahili kuhakikisha wanathamini mchango wa kituo cha Makumbusho kwa kufanyia
kazi eneo walilopewa na iwapo hawatakitumia ofisi yake inaweza kuwakabidhi watu
wengine wanaohitaji.
Akichangia juu ya
uanzishwaji wa kituo hicho aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Micheo na
Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili Dk. Mohammed Seif Khatibu, alipongeza wazo la
kuanzisha kwa kituo hicho kwani Kiswahili ni kitambulisho cha Watanzania na
lugha ya ukombozi wa nchi za Afrika.
Dk Aldin Mutembei
alisema nchi zote zinazojali historia na kuenzi maendeleo ya jamii, huweka
kumbukumbu na kuwajulisha watu wajue wanapotoka, walipo na wanapoelekea kwani asiyejua
anapokwenda huweza kupotea njia.
Alisema
ameshuhudia vituo kama hicho katika nchi mbalimbali ikiwemo Uholanzi,
Ujerumani, Denmark, Norway na Marekani katika jiji la Washington DC ambako kuna kituo kikubwa inachokusanya
taarifa za lugha na simulizi duniani.
Alisema kituo
hicho ambacho yeye ameteuliwa kushughulikia uanzishwaji wake, kitasaidia
kuhifadhi kumbukumbu za lugha ya Kiswahili na kwamba kuna utafiti unaofanywa
kuhusu maandishi ya Waafrika kabla ya ujio wa Waarabu unaofanyika hapa Tanzania.
“Wakoloni wana
kumbukumbu nyingi kuhusu maishayetu, hivi vituo nilivyovitaja, ukienda Berlin
kuna kumbukumbu nyingi kuhusu Kiswahili kuliko tulizonazo hapa Afrika
Mashariki, kwa hiyo kituo kama hiki kitawasiliana na vituo hivyo ili kurudisha
kumbukumbu hizo muhimu tulizozipoteza wakati wa Ukoloni” alisema Dk. Mutembei.
Kwa upande wake
Profesa Mugyabuso Mulokozi alisema wanahitaji kutafuta njia za kupata nyenzo
ili kituo kifanye kazi na kwa kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa na
kuhifadhi amali zake linatakiwa liwe jukumu la Serikali.
No comments:
Post a Comment