TANGAZO


Monday, July 29, 2013

Dar es Salaam kuwa Mwenyeji wa Maonyesho ya Vodacom Elimu Expo 2013


Mkurugenzi Mkuu wa Masoko Agencies (T) ltd, ambao ni waandaji wa maonesho ya elimu ya Vodacom Elimu Expo 2013, Joel Njama, akizungumza kuhusu kampuni yake hiyo pamoja na maonesho hayo. Katikati ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maonesho ya elimu ya Vodacom Elimu Expo 2013, yatakayofanyika kwa siku tatu Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Agosti 30 hadi Septemba Mosi. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Masoko Agencies (T) ltd, waandaji wa maonesho hayo, Joel Njama. 
 Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa akizungumza katika mkutano huo, kuelezea jinsi Kampuni yake ya Vodacom, inavyojali elimu hadi kusaidi baadhi ya shule umeme kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kimasomo. Katikati ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Masoko Agencies (T) ltd, waandaji wa maonesho hayo, Joel Njama.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (katikati), akiwa pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Masoko Agencies (T) ltd, waandaji wa maonesho hayo, Joel Njama, wakigonganisha glasi ili kuonesha mshikamano wao katika ushirikiano wa maonesho hayo ya elimu ya Vodacom Elimu Expo 2013, yatakayofanyika kwa siku tatu Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Agosti 30 hadi Septemba Mosi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo jijini leo. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Masoko Agencies (T) ltd, waandaji wa maonesho hayo, Joel Njama.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusu maonesho hayo.


Dar es Salaam, 29 Julai, 2013
Mji wa Dar es Salaam umeandaliwa kuwa mwenyeji wa maonyesho yaelimu ya kwanza ya aina yake mwaka huu, katika uwanja utakaoruhusu muingiliano na majadiliano kati yawatengenezaji wa sera, wapenda maendeleo, watunzi mbalimbali, wazazi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla. 

Maonyesho hayo yaliyopewa jina la Vodacom Elimu Expo, yanalenga kuwahusisha wadau wote wa elimu katika kuangalia mianya iliyopo, kugundua changamoto na kutafutia suluhisho ili kupelekea elimu bora kwaWatanzania kwa ujumla. 

Ni tukio litakalochukua siku tatu kuanzia tarehe 30 mwezi wa nane mwaka 2013 na litafanyikia viwanja vya michezo vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam. 

Wasemaji mbalimbali kutoka mashirika na viwanda tofauti wataongelea kuhusu viwanda vyao na vilevile kukutana na watu ambao wanapenda makampuni yao na bidhaa zao. 

“Maonyesho haya ya kujivunia yamepewa maudhui yasemayo ‘Elimu Bora ndio Tegemeo la Watoto wetu, Tuijenge kwa Pamoja.’ Tunawasihi wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya. Elimu ndio ufunguo wa maendeleo katika taifa hili kubwa, na kusaidia elimu katika nyanja tofauti ndio kubwatunaloweza kufanya”, alisema Njama, Mkurugenzi Mkuu wa maonyesho haya. 

Pia aliongezea kuwa wageni zaidi ya 150,000 wanatarajiwa kuhudhuria katika maonyesho haya, wakiwepopia wasanii na waburudishaji mbalimbali katika umati huo wa watu. 

Akiongea wakati akitangaza udhamini wa maonyesho hayo Dar es salaam, Kelvin Twissa, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, alielezea matumaini yake kuwa Vodacom Elimu Expo itasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu hapa nchini. 

Moja ya changamoto hizo kubwa ni ile ya kulipa ada ya shule, ambalo limeonekana ni jambo la kuchoshasana na kupoteza muda katika mistari mirefu ya benki. 

“Ni jambo la kusikitisha kabisa kuchelewa kulipa ada ya shule kwa sababu ya foleni zilizopo katika benkizetu. Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imekuja na njia ya kuitatua changamoto hii. Sasa hivi kuna uwezekano wa kulipa ada ya shule kupitia M-Pesa. Tunawasihi wadau wa elimu wanaomiliki shule kuanza kutumia huduma hii,” alisema Twissa. 

Maneno hayo pia yalisisitizwa na Mheshimiwa Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,ambaye pia alisema serikali ina jukumu la kuhakikishia elimu bora wananchi wake na katika hali ambayokila mtu anaweza kugharamia. 

“Hii ni fursa kwa wale wote ambao wanajadili na kuja na suluhisho ambalolitapelekea elimu Tanzania kuendelea katika njia iliyo bora. Serikali itatoa kila kinachohitajika ili kufanikisha jambo hili,” alisema Mulugo. 

Vodacom Elimu Expo, tukio lililoandaliwa na Masoko Agencies Tanzania Limited, ni tukio linalokusudia kushawishi ubora na mabadilishano ya habari na majadiliano ya kielimu ambayo yanalenga katika uboreshaji wa ngazi za kielimu Tanzania. 

Baadhi ya wadhamini wa maonyesho haya ni, Clouds FM, DTV, Entertainment Masters, Mwananchi Communications Ltd, Times FM, Primebiz Solutions Ltd, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). 

No comments:

Post a Comment