TANGAZO


Saturday, June 22, 2013

Wafuasi wa Renamo walaumiwa na serikali


Wapiganaji wa Renamo
Watu wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama cha Upinzani cha Renamo nchini Msumbiji.
Kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo shambulio hilo limefanywa siku mbili tangu msemaji wa chama hicho cha Renamo, Jeronimo Malagueta kutangaza kuwa kitafunga barabara kuu inayounganisha mji mkuu wa nchi hiyo na eneo la kusini lenye utajiri mkubwa wa madini.
Polisi walimkamata kiongozi huyo siku ya Ijumaa muda mfupi tu baada ya shambulio hilo kutokea.
Kundi hilo la waasi lilisaini mkataba wa amani mwaka wa 1992 ambao ulimaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyokuwa yamedumu kwa zaidi ya miaka kumi na sita.
Lakini kumekuwa na wasi mwasi kuwa mkataba huo wa amani uliosaini kwa pamoja na chama tawala cha Frelimo, huenda ukasambaratika, wakati kiongozi wa Renamo Alfonso Dhlakama, kurejea katika kambi yake iliyoko katika maeneo ya misitu ya milima ya Gorongosa kati kati mwa nchi hiyo.
Kiongozi wa Renamo Alfonso Dhlakama
Siku ya Jumatatu wanajeshi sita waliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, kushambulia kituo kimoja cha kuhifadhia silaha katika eneo la Dondo.
Ripoti zinasema kuwa watu hao walitoweka na kiasi kikubwa cha silaha iliyokuwa imehifadhiwa katika kituo hicho.
Chama cha Renamo hata hivyo kimekanusha kuhusika na shambulio hilo.
Chama hicho hakijasema lolote kuhusiana na shambulio la jana la mmoja wa washauri wakuu wa chama hicho Rahil Khan, alithibitisha kuwa Bwana Malagueta alikuwa anazuiliwa na polisi mjini Maputo.

No comments:

Post a Comment