Maelfu ya watu nchini Misri wameandamana mjini Cairo kumuunga mkono rais Mohammed Morsi.
Maandamano hayo yaliandaliwa na chama cha rais Morsi cha Muslim Brotherhood kwa ushirikiano na makundi mengine ya kiisilamu.
Waandamanaji walipiga mayowe wakilaani walichokiita upinzani ambao unapanga maandamano makubwa mwezi huu dhidi ya utawala wa rais Morsi.
Utakuwa ndio mwaka wa kwanza tangu kuingia mamlakani kwa rais Morsi atakayetawala kwa miaka mitano.
Waandamanaji hao wataandamana wakitaka kumshikiza rais Morsi.
Wadadisi wanasema kuwa maandamano ya kumpinga rais Morsi pamoja na yale ya kumuunga mkono ni ishara ya kuonyesha hali ya migawanyiko ilivyo kisiasa nchini Misri zaidi ya miaka miwili baada ya mapin
No comments:
Post a Comment