TANGAZO


Saturday, June 1, 2013

Polisi waondoka medani ya Taksim

 

Baada ya mapambano ya siku mbili na waandamanaji, polisi wameondoka katika medani ya Taksim mjini Istanbul na maelfu ya waandamanaji wameikalia medani hiyo.
Maandamano katika medani Taksim, Istanbul

Hapo awali waziri mkuu wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan, alitoa wito watu waache kuandamana haraka - maandamano makubwa kabisa kwa miaka kadha.
Lakini Bwana Erdogan ameahidi kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba polisi walitumia nguvu nyingi.
Nchi kadha zimeeleza wasiwasi kuhusu swala hilo.
Chanzo cha maandamano ni mpango wa kujenga maduka katika medani ya Taksim - mpango ambao Bwana Erdogan anasema atautekeleza.
Waandamanaji vijana piya wanailaumu serikali kwamba imekuwa ya kimabavu na kuifanya nchi kufuata Uislamu.
Msemaji wa serikali alikanusha malalamiko hayo alipohojiwa na BBC na alisema tuhuma zenyewe ni za kushangaza.

No comments:

Post a Comment