TANGAZO


Friday, June 21, 2013

Makamu wa Rais Dk. Bilal: Serikali inadhamiria kuvifufua viwanda vyote vya Tanga

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga leo Juni 21, 2013 kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo hilo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae na viongozi wengine kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, baada ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi la ujenzi wa viwanda katika eneo hilo wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa ramani ya ujenzi wa Viwanda hivyo, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa baadhi ya vifaa kama Solar Cooker, ambavyo ni baadhi ya vitakavyokuwa vikizalishwa katika Viwanda hivyo baada ya kukamilika, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.
Makamu wa Rais na baadhi ya Viongozi, wakishirikiana kurusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo.
Makamu wa Rais na baadhi ya Viongozi, wakishirikiana kurusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo, mjini Tanga leo.

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed Bilal (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo, mjini Tanga leo.


Na Mbonea Herman Tanga.
SERIKALI imesema itakifufua kiwanda kimoja baada ya kingine  ambacho kilikufa katika Mkoa wa Tanga, ili kuurudisha Mkoa huo katika hali nzuri ya kiuchumi iliyokuwepo wakati viwanda hivyo vikifanya kazi.

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohammed Bilali alitoa kauli hiyo leo katika sherehe ya kuweka jiwa la msingi kwenye eneo maalumu la uwekezaji la Tanga Economic Corridor lililopo Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga.

 Akitoa salamu za Rais kwa wananchi wa eneo hilo, litakalojengwa viwanda 17, Dk. Bilali alisema Serikali inataka kulifanya jiji la Tanga kuwa jiji la viwanda na kurejesha heshima ya mji huo Tanga .

''Napenda kutoa salamu maalumu kutoka kwa Rais, Serikali inadhamiria kulifanya jiji la Tanga kuwa la viwanda,katika miaka ya nyuma mkoa wa Tanga ulikuwa ukiongoza kwa kuwa na viwanda ,tunataka turudishe ile hali iliyokuwepo  miaka ya nyuma,"alisema Dk. Bilali.

Dk. Bilali alisema katika kuhakikisha tunavutia wawekezaji alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa sekta binafsi hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuifanyia marekebisho seria ya manunuzi na ile ya ubia kati ya serikali na wawekezaji kwa lengo la kuondoa ukiritimba uliopo.

"Tayari Bunge limeshafanyia marekebisho sheria hiyo na lengo la kufanya hivyo ni kuweka mazingira mazuri ya yatakayowavutia wawekezaji,''alisema, Dk. Bilali.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omari Nundu, alisema baadhi ya viwanda, vingi katika jiji la Tanga vimekufa huku akitolea mfano kilichokuwa kiwanda cha mbolea kilichopo Raskazone ambacho kilikuwa miongoni mwa viwanda vilivyokuwa vikiuinua mkoa wa Tanga kiuchuni.

Hata hiyo, akizungumza wakati akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda alisema atahakikisha katika kipindi cha utawala wake kila kiwanda kilichokuwa kikifanya kazi kinaendelea kufanyakazi kwa maslahi ya Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, akiwemo Misles Mbonela, alisema pamoja na kushukuru serikali kuwaletea viwanda ni vyema wakahakikisha wananchi wa eneo hilo, wanapewa kipaumbele.

Alitolea uzoefu wake katika shughuli za viwanda, Mbonela alisema wamekuwa wakitozwa fedha ili wapatiwe nafasi katika viwanda, hivyo swala ambalo wameiomba serikali kuhakikisha ukiritimba huo, hautokei katika viwanda hivyo.

Kwa upande wake, Juma Abdalla alisema wakati mwingine katika viwanda walivyokwisha fanyia kazi waligundua kwamba wanaowaathiri ni waswahili wenzao na wakati mwingine huwa hata mwekezaji anakuwa hafahamu ambacho wanafanyiwa.

Alisema wafanyakazi wengi wamekuwa wakihofia kutoa taarifa za ukiritimba uliopo na wanaofanyiwa wakihofia kupoteza vibarua vyao.

No comments:

Post a Comment