TANGAZO


Saturday, June 29, 2013

Blatter atetea FIFA



Sepp Blatter
Rais wa Fifa Sepp Blatter, anaamini kuwa hadhi ya shirikisho la mchezo wa soka duniani imeimarika kutokana na fainali za kombe la shirikisho, inayoendelea nchini Brazil, licha ya maandamano yanayoendelea nchini humo.
Akiongea kwa mara ya kwanza, tangu maandamano hayo kuanza, Blatter amesema anawahurumia raia wa nchi hiyo wanaoandamana katika miji mia moja nchini Brazil.
Maandamano zaidi yanatarajiwa kabla ya fainali za kombe hilo siku ya Jumapili kati ya Brazil na Uhispania katika uwanja wa Marikani mjini Rio.
Kuna wasi wasi mkubwa kuwa huenda rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff huenda asihudhuria fainali hiyo.
'' Fifa imekuwa na nguvu zaidi na hadhi yetu imeimarishwa. Mchezo wa soka umekuwa na nafasi kubwa miongoni mwa taifa hili na imewapa fursa ya kuelezea hisia zao'' Alisema Blatter.
Blatter amesema anawahurumia sana raia wa nchi hiyo kwa kuwa anafahamu masuala wanayoyapinga kupitia maandamano hayo ya amani na ameongea kuwa anatarajiwa serikali ya nchi hiyo itatatua masuala hayo kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la dunia itakayoandaliwa nchini humo mwaka ujao.

Maandamano yanayoendelea nchini Brazil
Shirikisho la mchezo wa FIFA limeshutumiwa sana nchini Brazil kwa kupata faida kubwa isiyotozwa ushuru kutokana na fainali za kombe la dunia kuandaliwa nchini humo, na kuiacha taifa hilo kuwekeza mabilioni ya fedha za umma bila manufaa yoyote.
Bwana Blatter hata hivyo amekanusha madai hayo.
''Dhamira kuu ya kombe la dunia sio kupata faida au kuchukua faida yote kutoka kwa nchi inayoandaa mashindano hayo, lakini ni kuisaidia taifa hilo ili kuhakikisha kuwa fainali hizo zinafanikiwa'' Alisema Blatter.
Blatter ambaye aliondoka nchini Brazil wiki iliyopita, huku maandamano hayo yakichacha, amepuuzilia mbali madai kuwa alitoroka Brazil hata bila kuwajulisha maafisa wengine wakuu wa Fifa.
Blatter amesema aliondoka Brazil ili kuhudhuria fainali za kombe la dunia kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 inayoandaliwa nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment