Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lymo (kushoto), akiongea na mwakilishi wa Kamati iliyoundwa ya maonesho ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa, Awamu ya kwanza, yaliyozinduliwa leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija - MAELEZO)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akisalimiana na mwakilishi wa Kamati ya maandalizi ya ufunguzi wa kusimamia mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa, Awamu ya kwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, akiingia katika viwanjwa vya Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam kuhudhuria ufunguzi wa maonesho ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa, Awamu ya kwanza.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal (kulia), akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lymo mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa, Awamu ya kwanza leo, jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanmzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), akisalimiana na mwakilishi wa Kamati ya kusimamia Mpango wa maendeleo.
Na Genofeva Matemu na Frank Shija – MAELEZO
WANANCHI wametakiwa kushiriki zoezi la utoaji wa maoni kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali juu ya njia bora ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya miaka mitatu, unaozihusisha sekta za Elimu, Maji, Miundombinu, Kilimo, Nishati na Madini pamoja na mapato ya Serikali.
Rai hiyo imetolewa leo, jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua maonesho ya upataji wa maoni ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa upataji wa matokeo makubwa ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo awamu ya kwanza
Amesema sekta sita muhimu zilizoteuliwa kuingia katika awamu ya kwanza zinatokana na mapendekezo yaliyotolewa na wataalam waliobobea katika nyanja mbalimbali walioainisha njia bora za ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ili kuharakisha maendeleo.
Rais Kikwete amewapongeza wataalam hao kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kupitia na kuchambua na kutoa mapendekezo ya namna bora ya utekelezaji ,mfumo huo utakaoleta matokea ya haraka katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Amefafanua kuwa mfumo huo pamoja na mambo mengine utatumika pia kupima utendaji kazi wa mawaziri, makatibu wakuu pamoja na watendaji wa serikali.
“ Mfumo huu utatupatia matokeo ya haraka kwa sababau utatuwezesha kufuatilia yale yote yanayofanywa na mawaziri ili kuona kama wamefikia au hawajafikia kile walichoahidi kukifanya”. Amesisitiza Rais Kikwete.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa mpango huo utaiwezesha wizara yake kuhakikisha kuwa suala la upatikanaji wa maji vijijini linatekelezwa na kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kusaidia vijiji kuanzisha kamati za watumia maji zitakazoshirikiana na Serikali kusimamia, kuratibu na kuendesha miradi hiyo katika maeneo yao.
Aidha serikali imekuwa na utaratibu wa kuainisha vipaumbele na kupanga mipango na utekelezaji wake toka awamu ya kwanza ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo serikali ilipambana na maadui watatu ambao ni Umaskini, Ujinga na Maradhi.

No comments:
Post a Comment