TANGAZO


Friday, May 24, 2013

Wataalamu wa Tiba za asili na mbadala wakutana jijini Dar es Salaam kujadili changamoto zinazowakabili

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Mohamed akifungua mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo, jijini Dar es salaam waliokutana kujadili mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali waliyonayo katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. (Picha zote na Aron Msigwa - MAELEZO)

Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba za Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Paulo Mohammed akitoa ufafanuzi wa hali halisi ya Tiba za Asili na Tiba mbadala nchini Tanzania na mpango wa Serikali wa kuendelea kuthamini huduma inayotolewa na wataalam hao, wakati wa mkutano wa Baraza la Wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.

Sehemu ya wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala  waliohudhuria mkutano wa Baraza la Wataalam wa tiba hiyo, wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo, jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Rose Shija akisoma salam za Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania, Dk. Rufaro Chatora leo, jijini Dar es Salaam ambaye amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kutatua changamoto zinazowakabili wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.


Mtafiti Mwandamizi Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Tiba Asili kutoka Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu, Hamis Masanja Malebo, akitoa mada kuhusu historia ya Tiba za Asili na uhusiano uliopo katika matumizi ya mimea ya asili kati ya tiba za asili  na tiba mbadala na tiba za kisasa katika utengenezaji wa dawa.


No comments:

Post a Comment