Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Simba Chawene akizungumza jambo na Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, wakati wa kikao cha Bunge leo, mjini Dodoma. (Picha zote na Zawadi Msalla - MAELEZO)
Mbunge wa Peramiho, mjini Songea, Jenista Muhagama akizungumza na Mbunge wa Mpanda Kaskazini, Ally Kessy katika kikao cha Bunge leo, mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiwaonesha Wabunge, moja ya michoro ya miradi mbalimbali ya umeme, wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti katika kikao cha Bungeni, mjini Dodoma leo.
Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, akiangalia moja ya michoro ya mradi wa umeme wakati bajeti ya Nishati na Madini, ikiwasilishwa Bungeni leo.
Mbunge wa Ubungo, mkoani Dar es Salaam, John Mnyika akisoma hotuba ya Nishati na Madini ya Kambi ya Upinzani kwenye kikao cha Bungeni, mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela akichangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Nishati na Madini kwenye kikao cha Bunge, mjini Dodoma leo.

No comments:
Post a Comment