Ofisa Elimu Wilaya Njombe mjini, Zegeli Leonard akikata utepe kuzindua ukumbi wa shule
ya Msingi na Ufundi Uwemba uliokarabatiwa
na Vodacom Tanzania, kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation)
kwa gharama ya shilingi Milioni 16. Wanaoshuhudia wa kwanza toka kushoto ni Mkuu
wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, Domician Mkama, na Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Robert Ngumbuzi.
Katibu Tawala, Wilaya ya Njombe, Evagry
Keiya (kushoto), akisalimiana na Mkuu
wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule, wakati wa
makabidhiano rasmi ya vifaa vya ujenzi vilivyotolewa msaada katika shule ya
Sekondari ya Anna Makinda, wilayani humo, vifaa hivyo vilivyogharimu Milioni 30, vilitolewa
na mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzani (Vodacom Foundation). Katikati ni
Mkuu wa shule hiyo, Veronica Mlozi.
Ofisa wa Vodacom Tanzania, Yessaya Mwakifulefule, akiwasalimu baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi na ufundi Uwemba Njombe,mara baada ya kuwasili
shuleni hapo kukabidhi ukumbi wa shule hiyo uliokarabatiwa na Vodacom
Foundation kwa kiasi cha shilingi Milioni 16.
Maafisa Vodacom Tanzania wakiwasalimu baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi na ufundi Uwemba Njombe,mara baada ya kuwasili
shuleni hapo kukabidhi ukumbi wa shule hiyo uliokarabatiwa na Vodacom
Foundation kwa kiasi cha shilingi Milioni 16.
No comments:
Post a Comment