TANGAZO


Monday, May 20, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Bilal ahani msiba wa Ally Sykes jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na OMR)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na baadhi ya wazee waliohudhuria shughuli za msiba, wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment