TANGAZO


Monday, May 20, 2013

Uzinduzi wa Wiki ya Fistula ulivyofana mjini Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Zaipora Pangani akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula leo mjini Bukoba. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacam Salum Mwalim. Wengine pichani kushoto ni Mwakilishi wa CCBRT Kasper Mmuya na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila.Maadhimisho hayo yanafadhiliwa na Vodacom, Vodafone na CCBRT. (Picha zote na Mpigapicha wetu))

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Zaipora Pangani akikabidhi funguo ya gari kwa Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA tayari kuanza safari ya kuanza Bukoba kwenda Dar salaam kupitia mikoa mbalimbali kuelimisha jamii juu ya tatizo la fistula yakiwa na ujumbe fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo katika hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone ya nchoini Uingereza.

Mwakilishi wa Taasisi ya CCBRT Kasper Mmuya akiongea kwenye hafla ya  uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula leo mjini Bukoba. Wengine pichani ni Kkatibu Tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Zzaipora Pangani, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA. Maadhimisho hayo yanafadhiliwa na Vodacom, Vodafone na CCBRT.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Zaipora Pangani akikabidhi funguo ya gari kwa Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA tayari kuanza safari ya kuanza Bukoba kwenda Dar salaam kupitia mikoa mbalimbali kuelimisha jamii juu ya tatizo la fistula na jinsi matibabu yanavyopatikana bila malipo katika hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.Kilelele cha maadhimisho hayo kitafanyika Mei 23 siku ya fistula duniani.

Wakazi wa Mji wa Bukoba waliofurika kushuhudia uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula uliofanywa leo mjini humo kueleka siku ya fistula duniani Mei 23. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na kufadhiliwa na Vvodacom, Vodafone na CCBRT yakiwa na ujumbe “Fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo.”


Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA akchana mistari kukonga nyonyo za wakazi wa mji wa Buko wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula uliofanywa leo mjini humo kueleka siku ya fistula duniani Mei 23. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na kufadhiliwa na Vvodacom, Vodafone na CCBRT yakiwa na ujumbe “Fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo.”

No comments:

Post a Comment