Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Seneta, Stive King, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo
katika jengo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku
nne katika jiji la Washington Dc, nchini Marekani, juzi Feb 6, 2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington Dc juzi, Feb 6, 2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington Dc, baada ya
mazungumzo yao yaliyofanyika juzi, Feb 6, 2013, Hoteli ya Omni Shoreham.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, nchini Marekani
katika jiji la Washington Dc, baada ya mazungumzo yao alipowasili jijini humo
kuanza ziara yake ya siku nne, iliyomalizika jana Feb 7, 2013. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wa tano kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi
Juma Maalim. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)





No comments:
Post a Comment