| Baadhi ya Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini, wakielekea katika ukumbi wa mkutano wa Bunge jana, mjini Dodoma. Maofisa hao, wamefanya ziara bungeni hapo, ili kuona shughuli mbalimbali za Bunge. |
Baadhi ya Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene (wanne kushoto, mstari wa mbele), wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge jana kuangalia shughuli mbalimbali za Bunge, mjini Dodoma.
| Baadhi ya Maofisa Habari na Mawasiliano Serikalini, wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana, wakifuatilia jinsi Bunge hilo linavyoendeshwa. |
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, akiwasilisha Azimio la Bunge la Kujiunga na Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio hilo limeungwa mkono jana katika mkutano wa kumi, kikao cha nane.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa (kulia), akiongea na Wabunge, James Mbatia (kushoto) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), katika viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana, baada ya Spika Anne Makinda (hayupo pichani), kutangaza rasmi kwamba Mitala ya Elimu inayotumika ni halali na ipo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisoma Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2012 katika ukumbi wa Bunge leo.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza wakati akikiendesha kikao hicho cha Bunge jana.
Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (kushoto) na Mbunge Joshua Nassari, wakitetea jambo wakati wa kikao hicho cha Bunge jana. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

No comments:
Post a Comment