TANGAZO


Friday, February 1, 2013

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara Phillip Mangula, asema Kigoma ya sasa sio ile ya zamani



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Komred Philip Mangula, akizungumza na wananchi wa Kigoma
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mangula akiteremka katika ndege.
Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mangula akisalimiana na Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, akisalimiana na baadhi ya makada wa chama hicho.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege, mjini Kigoma hii leo.
Makamu Mwenyekiti wa UWT, Dogo Mabruk (kushoto) na Mjumbe wa NEC-Wilaya ya Uvinza, Asha Baraka pamoja na wanachama wengine wa CCM wakimsikiliza Mangula.
Vijana wa CCM waliofika kumpokea Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Komredi Mangula, wakimsubiri kwa hamu, Uwanjani hapo. 

Na Mroki Mroki, FK BLG Kigoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula amewasili mkoani Kigoma asubuhi hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kupongeza mabadiliko makubwa yaliyopo mkoani humo hasa Uwanja huo wa Ndege ambao unaonekana sasa kuwa wa kisasa.

Mangula ambaye amepata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nappe Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambaye ni Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu. Issa Machibya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

Mangula amesema Kigoma ya sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi wanastahili pongezi kwa maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.

“Kigoma ya leo, sio Kigoma ile ya zamani ..Uwanja huu wakati ndege inataka kutua nilitaraji nitasikia matairi ya kihangaika lakini nikashangaa tunakwenda vizuri tu”, alisema Mangula akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.

Aidha, amewaambia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na mafanikio makubwa yaliyofikiwa hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa kigoma ambao zamani haukuwa na tabaka la lami ambapo sasa uwanja huo umewekewa tabaka la lami na kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata zamani wananchi wa Kigoma.

Pia Mangula amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli zinazoendelea kutolewa na wanasiasa wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma umesahaurika kitu ambacho amesema hakina ukweli kwani mkoa huo sasa umefunguka kwa miundombinu ya barabara.
Wakati huo huo, katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm, mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa ajili ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 3, 2013 katika uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia zaidi ya themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na wajumbe wa NEC na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua maandalizi hayo jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment