Mavazi ya watu nwaliouawa kwenye msongamano mjini
Abidjan.
Kisa hicho kilitokea kufuatia msongamano wa watu wakati wa sherehe hizo, za kuukaribishwa mwaka mpya wa 2013.
Vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema tukio hilo lilitokea mapema
alfajiri katika jiji kuu la Abijdan.
Wengi waliofariki ni watoto kati ya miaka minane hadi kumi na mitano.
Hata hivyo haijulikani kilichosababisha msongamano huo.
Ajali hiyo ilitokea katia uwanja wa michezo wa Felix Houphouet Boign, ambao una ukumbwa wa kuruhusu mashabiuki elfu sitini na tano wa soka na ulipewa jina hilo kama heshima ya rais wa kwanza wa nchi hiyo.
Kabla ya ajali hiyo uwanja huo uliandaa maonyesho ya muziki iliyohudhuriwa na mwana muziki kutoka Marekani Chris Brown.

No comments:
Post a Comment