
Mpiganaji wa M23 akiwa na chombo cha
mawasiliano
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limewawekea vikwazo
viongozi wa kundi la waasi wa M23 nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Umoja wa mataifa ulichukua hatua kama hiyo dhidi ya viongozi wa waasi wa
FDLR.
Kundi hilo la M23 lililoundwa na wanajeshi waasi,waliuteka mji wa Goma,
Mashariki mwa Congo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda, kutoka kwa wanajeshi
wa serikali na wale wa kutunza amani wa Umoja wa Mataifa.Waasi wa M23 washurutishwa kuondoka Goma
Lakini kufuatia shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa wapiganaji hao
walikubali kuondoka kutoka mjini humo mwezi uliopita.
Tangazo hilo limetolewa mkesha wa siku ya mwaka mpya siku moja tu kabla ya Rwanda kujiunga kuwa mwanachama wa baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili.
Umoja wa Mataifa na Serikali ya Congo, zimeishutumu serikali za Rwanda na Uganda kwa kuwaunga mkono wapiganaji hao wa waasi, madai ambayo yamepingwa vikali za serikali hizo mbili.
Rwanda inatuhumiwa kuunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupambana na wapiganaji wa waasi wa Kihutu ambao walitoroka nchini humo baada ya mauaji ya kimbari miaka ya tisini
No comments:
Post a Comment