Rais Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama, amewataka wabunge wa bunge la
wawakilishi kupitisha maazimio yaliopitishwa na bunge la Senate kuhusu sera mpya
ya uchumi bila kusita.
Rais Obama, amesema kuwa kwa mara ya kwanza wanaomiliki mabilioni na mamilioni ya fedha watalazimika kulipa ushuru unaohitajika kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
Wabunge wa chama cha Republican, wamesema kuwa watahitaji muda zaidi kusoma mapendekezo hayo.
Hata hivyo wantarajiwa kupiga kura baadaye hivi leo.

No comments:
Post a Comment