TANGAZO


Tuesday, January 1, 2013

Vijana wa Buguruni, Vingunguti walivyosherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013

Vijana kutoka maeneo ya Vingunguti na Buguruni wakiwa na ngoma zao, wakisherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013, usiku wa kuamkia leo, maenei ya Kwamnyamani, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
Vijana wa Buguruni Kwamnyamani wakiwasha moto katika shamrashamra hizo.

Vijana wakiwa wamepagawa, wakiukaribisha mwaka 2013, ulipoingia yapata saa 6 na dakika moja.

Hapa Vijana hao, wa Buguruni Kwamnyamani, Dar es Salaam wakiwasha fataki wakati walipokuwa wakisherehekea kuingia mwaka mpya wa 2013, usiku wa kuamkia leo.

Hapa fataki ikiwa inakolea moto na wenyewe wakishangilia kwa nguvu, wakati huo wa kuingia mwaka mpya wa 2013, usiku wa kuamkia leo.

Kundi la Vijana kutoka maeneo ya Vingunguti, wakiingia kwa shangwe maeneo ya Buguruni Kwamnyamani na kuchanganyika na vijana wa maeneo hayo, wakisherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013.

Vijana hao wakikata mitaa ya Buguruni Kwamnyamani, huku wakiserebuka kusherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013, usiku wa kuamkia leo.

Vijana kutoka maeneo ya Vingunguti na Buguruni Kwamnyamani, wakiwa wamechanganyika, wake kwa waume, wakisherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013.

Hapa vijana kutoka maeneo hayo, wakiwa na hamasa kubwa, wakishangilia kuingia Mwaka mpya wa 2013, usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam.
 
Vijana wa rika mbalimbali wa Buguruni Kwamnyamani, wakishangilia kuingia mwaka mpya wa 2013 katika maeneo yao hayo, usiku wa kuamkia leo.

Hapa vijana na wazazi wao, wakiwa maeneo ya nyumbani kwao, Buguruni Kwamnyamani, wakiangalia shamra shamra za kuingia mwaka mpya wa 2013.

Vijana hao, wakionesha furaha yao, wakati wa shamra shamra hizo kwenye mitaa ya Buguruni Kwamnyamani kusherehekea mwaka mpya wa 2013.

Vijana wakionesha kila ishara katika kuukaribisha mwaka mpya kwenye maeneo hayo.

Vijana wakiwa wamebeba vitu mablimbali kukamilisha furaha yao ya kusherehekea kuingia Mwaka mpya wa 2013.

No comments:

Post a Comment