TANGAZO


Tuesday, January 1, 2013

Matukio mbalimbali ya Kampuni ya Precision Air ilipomzawadia mchezaji bora wa Afrika wa BBC, Christopher Katongo wa Zambia













Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM,
SHIRIKA la ndege nchini, Precisionair, limemzawadia mshindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2012, Christopher Katongo, tiketi ya kwenda na kurudi kwa watu wawili sehemu yoyote ambapo ndege hiyo inafanya safari zake.

Precision Air ilikabidhi tiketi hiyo jijini Lusaka kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam.

Precision Air pia ilitoa punguzo kwa tiketi za wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia ambao walikuwa walikuja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika Desemba 23, 2012.

Katika makabidhiano hayo ambayo yalifanyika kwenye uwanja wa ndege wa jijini Lusaka muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ambayo ilihudhuriwa na balozi wa Zambia nchini Tanzania, Bi. Grace Mujuma, Bi. Chiza alisema Shirika la Precision Air limemzawadia tiketi Katongo kwa kuwa balozi mzuri ndani na nje ya bara la Afrika. 

Mchezaji bora wa Afrika ataweza kuzitumia huduma za shirika letu la Precisionair na pia kulitangaza ndani na nje ya bara letu la Afrika.

Shirika hilo la Precision Air linafanya safari zake katika miji ya; Lubumbashi - Kinshasa - Dar na Kinshasa –Harare, Lusaka, Kisangani - Kigali – Entebbe, na Comoro. 
Katongo, amenyakua zawadi ya tiketi toka Precision Air wiki kabla ya kutua nchini, baada ya kutangazwa mshindi wa Tuzo hizo za BBC za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2012 huku akiwapiku wachezaji nguli wenye majina makubwa duniani kama vile; Didier Drogba, Yaya Toure, Demba Ba na Younes Belhanda.

Licha ya Katongo kunyakuwa ushindi wa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2012, ambapo pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo ambao pia ni mabingwa wa Afrika ilinyukwa bao 1-0 na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Bao la Stars liliwekwa kimyani na Mrisho Ngassa.

Katongo, alizaliwa Agosti 31, 1982 katika mji wa Mufulira, Zambia ambapo hivi sasa anacheza katika klabu ya Henan Construction kama mshambuliaji.

No comments:

Post a Comment