Wahisani au wafadhili wa kimataifa, wanaokutana nchini
Ethiopia, wametoa ahadi za kuchagia bajeti ya dola milioni 950, inayotarajiwa
kufadhili kampeini ya kimataifa ya kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu nchini
Mali.
Wanatarajiwa kuweka juhudi zao sana katika mji wa Kidal ambayo ni ngome ya wapiganaji
Kongamano la wafadhili wa kimataifa, linafanyika mjini Addis Ababa Ethiopia.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara alisema kuwa bajeti ya majeshi ya kimataifa, itafikia dola milioni 950, zaidi ya mara mbili ya makadirio yaliyowekwa na Muungano wa Afrika.
Muungano wa Afrika uliahidi kutoa dola milioni tano, kwenye mkutano huo siku ya Jumatatu na ilitarajiwa kuwa Umoja wa mataifa pamoja na wahisani wengine 60 au 70 walioalikwa kwenye kongamano hilo wangeweza kutoa ahadi zao kusaidia kampeini hiyo.
Kulingana na orodha ya wale ambao tayari wameahidi kutoa msaada, Japan aliahidi kutoa dola milioni 120, Marekani dola milioni 96 na Ujerumani dola milioni 20.
Pesa hizo zitatumika kwa msaada wa kibinadamu kwa vikosi vya Afrika, kuboresha usalama na mustakabali wa Mali.
Mwenyekiti wa tume ya Muuungano wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, aliwaambia wajumbe kuwa walikuwa wamejumuika kuunga mkono Mali na watu wake.
No comments:
Post a Comment