TANGAZO


Sunday, January 27, 2013

Soko la Bujumbura lateketea

 
Nchini Burundi soko kuu la mji mkuu Bujumbura limeteketea kwenye moto asubuhi mapema ya Jumapili.
 
Bujumbura, Burundi

Soko hilo ndilo kubwa kuliko yote nchini humo.
Sababu za kuzuka moto huo hazijajulikani bado.

Wafanyabiashara wamelaani kuchelewa kwa shughuli za uokozi ambapo gari za kuzima moto zimefika mahala pa tukio saa mbili baada ya moto kuripuka.

Mwandishi wetu mjini Bujumbura anasema wachuuzi wengi akina mama wamepoteza mali yao yote.

Kumekuwa na ripoti kwamba wakati moto unawaka baadhi ya watu wamepora mali katika soko hilo.

No comments:

Post a Comment