Wanajeshi wa Ufaransa wanasonga mbele kuelekea mji wa
Timbuktu ulioko katika jangwa la kaskazini mwa Mali, moja kati ya miji michache
iliyobaki mikononi mwa wapiganaji wa Kiislamu.

Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema Wafaransa wanatarajiwa kuikomboa Timbuktu bila ya tatizo.
Ndege za Ufaransa piya zimeshambulia mji wa Kidal ambako ndiko wapiganaji walianza uvamizi wao mwezi Machi mwaka jana.
Jumamosi wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa mji wa Gao uliokuwa ngome ya wapiganaji.
Na Mali ndio swala muhimu linalojadiliwa kati ya viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, AU, wanaokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Sasa nchi zaidi za Afrika zinatarajiwa kuchangia wanajeshi katika kikosi cha kimataifa kitachokwenda Mali, mbali ya wale walioshafika nchini humo.
No comments:
Post a Comment