Wasanii wakilishusha jeneza lililobeba mwili wa marehemu msanii wa filamu nchini, marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI), kwenye makaburi ya Kisutu, tayari mazishi jijini Dar es Salaam leo. |
Rais Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la msanii wa filamu, marehemu Sadik Juma Kilowoko, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. |
Baadhi ya wasanii wakiwa na watu mbalimbali waliohudhuria mazishi ya msanii Sadik Juma Kilowoko kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. |
Rais Kikwete akishuhudia safari ya mwisho ya Msanii wa Filamu nchini Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Kisutu jijini Dar es Salaam. |
Waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali wakati wa maziko ya msanii huyo. |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akihojiwa na waandishi wa habari kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya mazishi ya msanii Sadik Juma Kilowoko. |
Rais Kikwete akiwasili kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kwenye safari ya mwisho ya msanii wa Filamu nchini, Sadik Juma Kilowoko 'Sajuki'. |
Jeneza la mwili wa marehemu Sadik Juma Kilowoko, lipelekwa kwenye gari tayari kwenda makaburi ya Kisutu kwa mazishi leo. |
Waombolezaji wakisoma dua muda mfupi kabla ya kuondoka nyumbani kwake kuelekea Makaburi ya Kisutu kwa mazishi. |
No comments:
Post a Comment