TANGAZO


Saturday, January 12, 2013

Mwanajeshi apasuka kichwa baada ya lori lao kujipigiza na mti mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam

 
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya na kupasuka sehemu za kichwani wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07, aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora, karibu na Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jioni hii.
 
Wasamaria wema wakiwa wamembeba kijana aliyepasuka kichwa akiwa kwenye lori la Jeshi.
Baadhi ya wasamaria wema wakimpeleka Hospitali majeruhi huyo.
Wasamaria wema wakihangaika kutafuta gari la kumpeleka Hospitali.
Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa Hospitali.
 
Lori aina ya IVECO, ambalo majeruhi huyo, alikuwa amepanda huku likiwa limesheheni mizigo.
 
Akiingizwa kwenye Bajaj kwa ajili ya kukimbizwa Hospitali.
Lori alilokuwemo majeruhi huyo na kupata nalo ajali, likiwa katika maeneo ya ajali hiyo.
Wananchi wakilishangaa lori hilo, lililokuwa likipita barabara ya Samora kwa kupita sehemu ya njia moja (No Entry) ya mtaa huo. 
Hii ndiyo Barabara ya Samora, ilipotokea ajali hiyo.
 
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka sehemu za kichwani.

No comments:

Post a Comment