TANGAZO


Saturday, January 12, 2013

Rais Shein akagua gwaride, alihutubia Taifa, Kilele cha Maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi, Mjini Zanzibar

Wananchi wa Zanzibar kutoka Mikoa mbalimbali wakiwa katika kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,  zilizofanyika leo, Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali ya Zanzibar wa wakiwa katika kilele cha Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika leo, Uwanja wa Amaan Mjini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua kikosi cha wanawake cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakati wa maadhimisho hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua kikosi cha wanaume cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakati wa maadhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakati wa maadhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipomaliza kukagua vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, uwanja wa Amaan, Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma, alipowasilikatika Uwanjawa Amaan
kwenye maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimianana Rais Jakaya Kikwete, alipowasili Uwanja wa Amaan kwenye maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, alipowasili katika Uwanja wa Amaan
kwenye maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  mama Mwanamwema Shein na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Davis Mwamunyange, wakiwa jukwa kuu la Uwanja wa Aman wakati wa maadhimisho hayo. 
Waziri Mkuu Mstaafu Lowasa,Mama Shadya Karume na
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, wakifuatilia kwa makini ratiba ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katik sherehe za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Mjini Zabzibar, wakisikiliza hotuba ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduizi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungia wananchi waliokuwa wakipita kwa maandamano uwanjani hapo. Kushoto aliyekaa ni Rais Jakaya Kikwete, akifuatilia matukio ya sherehe hizo.
Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakipita mbele ya Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi, DkAli Mohamed Shein kwa Maandamano ya Sherehe za Kilele cha Miaka 49 ya  Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika leo, Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZWanawake kikipita mbale ya Rais kwa Gwaride la Mwendo wa pole,katika sherehe za Kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matiukufu ya Zanzibar huko Uwanja Amaan Studium, Mjini Zanzibar leo.
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Wanawake, kikipita mbale ya Rais Dk. Shein kwa gwaride la mwendo wa pole, katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan, Unguja leo.
Kikosi cha Jeshi la Mafunzo la Serikali ya Mapinduzi, Wanaume kikipita mbale ya Rais Dk. Shein kwa gwaride la mwendo wa pole, katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar leo.
Kikosi cha Bendera cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),  Wanaume, kikipita mbale ya Rais wa Zanzibar, Dk. Shein kwa gwaride la mwendo wa haraka katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar leo.
Kikosi cha Jeshi la (KMKM), Wanaume kikipita mbale ya Rais Dk. Shein kwa gwaride la mwendo wa haraka, katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan  Mjini Unguja leo.
Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Wanaume kikipita mbale ya Rais Dk. Shein kwa gwaride la mwendo wa haraka, katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Amaan, Mjini Unguja leo.
Kikosi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikipita mbele ya Rais Shein kwa gwaride la mwendo wa kurukaruka, katika maadhimisho hayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduizi Dk.Ali Mohamed Shein, akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar kupitia katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapunduzi Matukufu ya Zanzibar huko Uwanja wa Amaan Studiuma Mjini Zanzibar leo, kuhudhuriwa na Maelfu ya wananchi mbali mbali Mjini na Mashamba.



Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar      12/01/2013

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema mafanikio yote yaliyopatikana Zanzibar katika kipindi cha miaka 49 na miaka ijayo kwenye nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa msingi wake mkubwa ni Mapinduzi ya Januari 1964.

Amesema mafanikio zaidi yatapatikana iwapo Wananchi wataendelea kudumisha mshikamano na amani iliyopo Zanzibar pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo Zanzibar.

Rais Shein ameyasema hayo leo, alipokuwa akilihutubia Taifa katika kilele cha sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Amesema ushirikaiano wa Serikali na wananchi umeipatia Zanzibar mafanikio mazuri katika kuimarisha uchumi wake ambao mwenendo wake umeliwezesha pato la Taifa kufikia Shilingi Bilioni 1,198 mwaka 2012 kutoka Bilioni 946 mwaka 2011.

Amefahamisha kuwa mafanikio hayo yametokana na kukua kwa Sekta ya Uvuvi, Biashara na ujenzi wa Mahoteli na Mikahawa jambo ambalo limesaidia Serikali kupunguza mfumko wa bei kutoka asilimia 20 mwaka 2011 hadi asilimia 4.2 mwaka 2012.

Kuhusu Kilimo Rais Shein amesema Serikali yake inaendelea kuchukua juhudi mbali mbali za kukiendeleza kilimo ikiwemo kuimarisha Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili kuhakikisha kuwa Hekta 8,521 za Unguja na Pemba zinatumika kwa ajili ya kilimo hicho.

Aidha ameongeza kuwa Serkali inaendelea na azma yake ya kulinda hadhi ya zao la Karafuu ambapo mkakati wa kupatikana kwa Utambulisho maalum wa Karafuu za Zanzibar (Branding) upo katika hatua nzuri.

Amewahimiza Wakulima kupanda Mikarafuu kwa wingi na kuyatunza mashamba yao na kuachana na tabia ya kuuza Karafuu kwa njia ya magendo.

Kuhusu maslahi ya Wafanyakazi Dkt. Shein amesema Serikali inaendelea kuimarisha maslahi bora kwa watumishi wote na kuimarisha mishara na stahili nyingine za wafanyakazi kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu ili kuendesha vyema maisha yao.

Kuhusu Muungano Dkt. Shein amewahakikishia wananchi wote kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza Muungano huo na kuwatumikia wananchi wote.

Akitoa salamu zake Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe hizo ambaye pia Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd amesema jumla ya Miradi ya kimaendeleo 53 yenye thamani ya Shilingi 97.4 Bilion imezinduliwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Awali Rais Shein alipokea Salamu za Rais na Gwaride maalum kutoka Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja Vikosi vya SMZ, Maandamano ya Wananchi na Taasisi mbalimbali za Serikali ambapo pia Jumla ya Mizinga 21 ilipigwa kuhanikiza sherehe hizo.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na Viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete,Makamo wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd, Marais wastaafu, Mawaziri, Mabalozi, Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment